Wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi ya Chalinze mkoani Pwani wamehimizwa kusoma kwa juhudi ili kutengeneza maisha yao ya baadaye huku wakipewa changamoto ya kujitahidi kila wakati kuwa bora katika masomo yao na kwa kila kitu wanachofanya.

Hamasa hiyo imetolewa mapema wiki na Meneja wa Benki ya Kitaifa ya Biashara (NBC) Tawi la Samora Bi Zubeider Haroun wakati akikabidhi mifuko 75 ya saruji kwa shule hiyo ikiwa ni hatua ya benki kuboresha miundombinu shuleni hapo hususani kwa kujenga choo cha wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Bi Zubeider aliwasihi wanafunzi hao kuwa elimu inaweza kuwapeleka mbali na kutimiza ndoto zao, kwa hivyo wanahitaji kusoma kwa juhudi katika masomo yao huku akiwasisitiza kutokata tamaa hasa wanapopata changamoto katika safari zao za masomo.

“Kwa hivyo nawasihi muweke juhudi katika masomo yenu ili kwa ajili ya faida ya maisha yenu ya baadae kwa kuwa elimu ni ufunguo ambao unafungua milango ya maisha yote. ” alisisitiza

Aliongeza kuwa benki hiyo itaendelea kusaidia maendeleo ya Elimu na ikiwemo kwa wale walio na mahitaji maalum ili kuboresha mfumo wa elimu jumuishi nchini.

“Kama benki tumejitolea kabisa kusaidia ujenzi wa hitaji hili muhimu la miundombinu ya katika shule hii ili kuboresha upatikanaji wa elimu hususani kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum.’’ Alisema.

Pia, Bi Zubeider alitoa wito kwa taasisi zingine na watu binafsi kuchangia kwa shule na vituo vya elimu kama nguzo muhimu kuelekea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Akipokea msaada huo Bi Aufemia Ngweta, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo aliishukuru Benki ya NBC kwa msaada huo na utashi wake katika kusaidia ukuaji wa elimu katika Wilaya hiyo. Pia alitoa wito kwa wadau zaidi kusaidia shule hiyo.

"Hapa shuleni kuna watoto wenye ulemavu tofauti, kuna wale walio na ugonjwa wa kupooza kwa ubongo ambao wanahitaji vifaa vingi vya kuchangamsha akili zao ili waweze kujifunza vitu mbalimbali kama ufundi na ujuzi mwingine kwa maendeleo yao ya baadaye. Kwa hivyo juhudi zaidi zinahitajika kuhakikisha tunawafundisha vyema. ”Bi Ngweta alifadhaika

Alimshukuru pia Bi Zubeida kwa kuwahamasisha wanafunzi hao, akibainisha kuwa ni matumaini yake wanafunzi hao watabadilisha mawazo yao na kuthamini kwamba watu wenye mahitaji maalum wanaweza kuishi na kufaulu maishani hususani kupitia elimu.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Chalinze walishukuru Benki hiyo kwa msaada huo huku wakiaahidi kufanya vizuri kitaaluma sambamba na kutoa wito kwa jamii iendelee kuwasaidia ili waweze kutimiza ndoto zao.
Maofisa wa benki ya NBC tawi la Samora wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Chalinze na Wawakilishi wa Umoja wa Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) walipokwenda kukabidhi msaada wa mifuko ya saruji kwa ajili ya Ujenzi wa Vyoo kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum shuleni hapo.
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Samora Bi Zubeider Haroun (kulia) akimshukuru Mwalimu Mkuu Msadizi wa Shule ya Msingi Chalinze Bi Aufemia Ngweta (kushoto) wakati wa kukabidhi Msaada wa Mifuko ya saruji iliyotolewa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na Umoja wa Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa ajili ya kuboresha Miundombinu ya Vyoo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum shuleni hapo.
Meneja wa NBC tawi la Samora Bi Zubeider Haroun akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji iliyotolewa na Benki hiyo kwa kushirikiana na Umoja wa Wanafunzi wa Chuo cha Udhibiti wa Fedha (IFM). Msaada uliotolewa utasaidia kuboresha miundombinu katika Shule hiyo hasa jengo la Vyoo vya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...