Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma

MGOMBEA urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Pombe  Magufuli kesho Septemba 28 mwaka huu anatarajiwa kuendelea na mikutano yake ya kuomba ridhaa ya Watanzania ili aweze kuchaguliwa na kuongoza nchi kwa miaka mitano mingine.

Akizungumza leo Septemba 27, 2020 Mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole amesema Dk.Magufuli ataendelea na mzunguko wake wa mikutano ya kampeni ambayo anaitumia kuomba ridhaa kwa watanzania ili ikifika Oktoba 28 mwaka huu wamchague tena aendelee kufanya kazi ya kuleta maendeleo.

"Kesho atandelea na safari yake ya kampeni ambapo ataondoka katika Jiji la Dodoma kuelekea Iringa, atakuwa na mikutano ya njiani, kwani uzoefu unaonesha mara nyingi wananchi hujitokeza, hivyo mgombea wetu hutenga muda kuwasilimu na kuwoamba kura.

"Pia hutumia mikutano hiyo kuwaombea kura wagombea ubunge na wagombea udiwani wa Chama chetu .Atatumia gari na atakapofika Iringa atakwenda moja kwa moja Uwanja wa Samora ambako atakuwa na mkutano mkubwa kabisa, utakuwa mkutano wa hadhi ya mkoa.

"Atakuwepo yeye na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi, viongozi wa CCM Mkoa wa Iringa, wagombea wote wa ubunge na madiwani wote.Watakuwepo wana CCM na Watanzania kwa ujumla.

"Nitumie nafasi hii kwa niaba ya Chama chetu kuwaomba wananchi wote kuja kwenye mkutano, kusikiliza maoni ya mgombea , maono ya Chama pamoja na sera za wapi tunakotaka kwenda katika kuleta maendeleo ya Taifa letu,"amesema Polepole.

Wakati huo huo Polepoe amesema Dk.Magufuli Septemba 29 ataelekea mkoani Mbeya na kabla ya kufika huko atakuwa na mkutano mkubwa Njombe pale Makambaku na kote huko atakuwa akifanya mkutano."Siku ya Septemba 30 atakuwa na mkutano mkubwa kabisa Mbeya. Hivyo wananchi wa Mbeya tunawakaribisha katika mkutano huo.

"Tunaendelea kusisitiza wale ambao wamekuwa mashuhuda wa mikutano ya  CCM inavyojaza watu, sera nzuri na maoni ambayo yamekuwa yakitolewa, tunaomba Oktoba 28 mumchague Rais wa CCM, wabunge na madiwani wa CCM ili tutengeneze utatu mtakatifu na hatimaye kuendelea na shughuli za maendeleoe ya nchi yetu,"amesema.

Akizungumza zaidi kuhusu kampeni za Chama hicho, amesema kesho Septemba 28 mwaka huu wanaanza kuhesabu mzunguko mkuu wa kampeni zao wa siku 30 na kwa kutumia siku hizo mgombea wao atajikita kutoa maelezo yaliyosheheni ushahidi, takwimu kwa maana ya tulikotoka, tuliko na tunakokwenda.

"Tulikotoka tunapafahamu, tulipo tunakufahamu na tunakokwnda Ilani ya CCM imeshatoa maoni .Katika siku hizo 30 mbali ya kuwa na maono ya Chama , pia mgombea wetu ambaye tunamuamini atatukuwa akitumia mikutano hiyo kutoa maono yake na sera za kule ambako anatamani kuona Taifa linakwenda kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Watanzania wote.

Hata hivyo amesisitiza umoja, amani na mshikamano ndio ambao wataendelea kuelezea kwa wananchi, na kwamba hawatumia jukwa la mgombea wao urais kujibu watu, lakini chini ya Katibu Mkuu Dk.Bashiru Ally, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na timu zima ya kampeni itajibu hoja mbalimbali za uongo, uzushi na upotoshaji unaofanywa na wagombea wa vyama vya upinzani.

Pia amesema siku ambazo zimebakia za kufanya kampeni wataongeza injini nyingine kwa ajili ya kuongeza mashambulizi ya kushambulia kwa kufanya siasa safi na za kistaarabu."Tutakwenda kwenye Kata na kushuka huko kwa mtindo wa kushambulia, Watanzania watarajie ujumbe wa kudumisha amani na mshikamano, amani iliyopo iendelee kulindwa,"amesema Polepole.
MGOMBEA urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Pombe  Magufuli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...