Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mbeya 

MGOMBEA ubunge jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Tulia Ackson amesema wananchi wa Mkoa wa Mbeya wameshaamua uchaguzi mkuu mwaka huu kura zote za urais zitakwenda kwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama hicho Dk.John Magufuli na sababu za kumchagua wanazo. 

Akizungumza leo Septemba 30 mwaka 2020 mbele ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya , Dk.Tulia amemwambia Dk.Magufuli kwa umati ambao umejitokeza kwenye mkutano huo wa kampeni ni uthibitisho tosha sio tu Mbeya Mjini bali ni Mkoa wote wa Mbeya ni wa kijani na wao wameshaamua kura zote ni kwa Dk.Magufuli. 

"Naamini umati huu wagombea wote wa ubunge na udiwani watashinda na mimi nitashinda, wenzangu wamezungumza mambo makubwa ambayo yamefanyika na wewe mgombea wetu kupitia CCM ndio umefanya.Hoja tunazo kwanini tutakupa kura mgombea wetu Dk.Magufuli,"amesema. 

Akizungumzia baadhi ya mafanikio ambayo yamepatikana katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Dk.Magufuli ni kwamba Sh.bilioni 31 katika elimu ya msingi na sekondari na kwamba fedha hiyo ni nyingi.Katika elimu bure kwa shule za msingi Sh.bilioni tatu zimetumika kulipia watoto ili wapate elimu."Sisi tuna hoja wezetu wana vihoja. Kwa sekondari Sh.bilioni 13 zimeingia kwa ajili ya elimu bure, tunampongeza mgombea wetu wa urais lakini tuna ahadi kwake tutampa kura. 

"Katika elimu ya juu Chuo cha Mzumbe tumepatiwa Sh.bilioni tatu, chuo cha Sayansi na Teknolojia nako kimeboreshwa, tumepewa Sh.bilioni saba kwa ajili ya miundombinu, katika elimu Rais Magufuli ametenda haki, na katika elimu kuhusu Mbeya Mjini tutawapuuza watu wanaosema kuwa serikali wanaangalia maendeleo ya vituo . 

"Watoto wanaosoma elimu bure ni maendeleo ya watu sio vitu.Katika afya Mbeya Mjini tumepata fedha nyingi kwani Sh.bilioni1.3 tumepata kwa ajili ya vituo vya afya.Hospitali ya Mkoa imeshapata Sh.bilioni 3.7 na yapo mambo makubwa yanaendelea pale hospitali ya kanda ambayo imekamailika na vifaa vyote viko pale. 

"Sisi Mbeya tutamchagua Dk.John Magufuli tunapozungumzia afya hatuzungumzi vitu bali tunazungumzia afya zetu, hatuwezi kusema Dk.Magufuli anafanya maendeleo ya vitu na sio watu, tutawapuuza watu hao ambao wamekuwa wakitoa lugha za kututengenanisha.Katika miundombinu Sh.bilioni 31 zimetumika kuboresha miundombinu.Kazi kubwa ambayo imefanyika tunaiheshimu, katika eneo la miundombinu katika uwanja wa ndege zaidi ya Sh.bilioni 20 zimeingia. 

"Wametoka watokapo na ndege wakapita katika barabara za Magufuli, wamekuja hapa kutuongopea, hatukubali tutawapuuza.Dk.Magufuli amefanya maendeleo katika maeneo yote ambayo ni kipimo cha maendeleo, hivyo tunaposema tunao utayari maana yake mambo makubwa tumeyaona, yale ambayo tunayatarajia tunaamini yatafanyika,"amesema Dk.Tulia. 

Pia amesema kuna miradi mikubwa ambayo itafanyika iwapo wananchi watamchagua Dk.Magufuli huku akieleza kuwa maji kutoka Kiwira hadi Mbeya Mjini Sh.bilioni 70 zitatumika. "Nataka nione wale ambao watampa kura Dk.Magufuli, naamini tutayaishi yale yote ambayo tumeyazungumza". 

MGOMBEA ubunge jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Tulia Ackson

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...