Na Said Mwishehe, Michuzi TV 

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole amesema amefurahishwa na taarifa za CHADEMA na ACT Wazalendo kutaka kuungana ili kumsimamisha mgombea mmoja kwa nafasi ya urais.

Akizungumza leo Septemba 25, 2020 Mjini Dodoma Polepole amesema kwamba amesikia Bernard Membe upande wa pili wamemuonda kwenye nafasi ya kugombea urais."Nasikia wamekula kichwa upande wa pili.

"Nimefurahi sana, na naamini tutawachapa wale mapema asubuhi wakiwa wameungana hivyo hivyo na mimi nawashauri wasisubiri Oktoba 3 , waungane from now(waungane sasa), halafu ndio watajua tulikotoka na watanzania hawa miaka mitano iliyopita,"amesema Polepole.

Amefafanua kuwa Rais ameingia katika nchi hii ikiwa masikini,lakini Rais Magufuli kapambana na nchi yetu imefikia uchumi wa kati."Mzee huyo amepambana tumefanikiwa, kwa msaada wa Mungu wa mbinguni na kujitoa kwa haki kwa Rais Dk.John Magufuli".

Wakati huo huo Polepole amesema Membe katika moja ya mkutano wake amesikika akisema ataruhusu kangomba."Anajua maana yake nini, mtu amekuwa kwenye dhamana ya kimataifa kwa miaka nane, anashindwa kuelewa ulanguzi?

"Anashindwa kuelewa ulanguzi?Anaweza kufanya kazi gani, walanguzi warudi kwenye biashara ya korosho ambao wanawalalia wafanyabiashara ya korosho, halafu yuko mstari wa mbele,"amesema Polepole.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...