*Wakaguzi wa Ngozi kutangazwa gazeti la serikali ili kuwapa mamlaka

Na Chalila Kibuda,Michuzi T
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imesema kuwa serikali imedhamiria kusimamia bidhaa ya ngozi ili kuleta maendeleo nchini.

Bidhaa ya ngozi imekuwa hainekani katika mchango wa kutokana na bidhaa hiyo kuandaliwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na mifugo iliyopo nchini.

Akizungumza Kwa Niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel katika Mafunzo ya Waweka Madaraja ya Ngozi uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe Gabriel Bura amesema kuwa Tanzania ni nchi ya pili kwa idadi ya Ng'ombe Barani Afrika kwa kuwa na Ng'ombe Milioni 32.2 huku ikiongozwa na Ethiopia Milioni 52.

Amesema kuna viwanda viwili vinavyosindika ngozi kufikia hatua ya mwisho ambavyo ni Himo Tannery pamoja na Moshi Leather Industry Ltd vyenye uwezo kusindika futi za mraba 15000 hadi 10000 ni sawa vipande 1000 kwa Ng'ombe 9000 na Mbuzi uzalishaji ngozi 31000 lakini ni asilimia 10 ya ngozi zinazopelekwa viwandani na asilimia 90 hazifai kushindikwa kutokana na kukosa ubora.

Amesema kazi ya kiwanda sio kuchagua ngozi kwani zinatakiwa ngozi hizo zifanyiwe ukaguzi tangu zoezi la uchinjaji na uchunaji.

Bura amesema kuwa utaratibu kwa kuanzia sasa wachunaji wote wanatakiwa kuwa la leseni kutoka katika wizara hiyo.

Amesema katika sheria iliyopo wakaguzi wote ngozi wanatakiwa kutangazwa katika gazeti la serikali ili kuwapa mamlaka kwa kuwa kitambulisho katika kuepuka watu.Aidha amesema serikali imewekeza katika kiwanda cha ngozi katika Gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro hivyo uwekezaji huo unatakiwa kuleta matokeo chanya katika sekta ya ngozi.

Mshiriki wa Mafunzo hayo kutoka kiwanda cha ACE Godson Shayo amesema utaratibu wa serikali katika usimamizi ngozi utaleta tija na matokeo kuweza kuonekana.

Kwa upande wa Mkaguzi wa Ngozi Kutoka Manispaa ya Ilala Khalifa Kondo amesema mafunzo hayo yana umuhimu sana.


Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo ,Usalama wa Chakula na Lishe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Gabriel Bura akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Waweka Madaraja ya Ngozi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Mshauri Mwelekezi wa Ngozib Emmanuel Muyinga akitoa maelezo kuhusiana na utaratibu wa uwekaji madaraja katika ngozi katika mafunzo ya uwekaji madaraja katika ngozi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Mshiriki wa Mafunzo ya Wawekaji Madaraja ya Ngozi wa Kiwanda cha Usindikaji Ngozi cha ACE Godson Shayo akizungumza umhimu wa mafunzo hayo namna yatavyoleta matokeo chanya.

Mkurugezi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo,Usalama wa Chakula na Lishe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi akionesha bidhaa za ngozi zinazozalishwa nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...