Mwenyekiti wa Machinga Soko la Sabasaba Elizabeth Siame akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusu mambo makubwa waliyofanyiwa na Dk John Magufuli ya kimaendeleo.

Katibu Muenezi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Henry Mwenge akipokea salamu za wamachinga wa mkoa huo walizozitoa kwa Mgombea Urais wa CCM na Rais Dk John Magufuli kwa kuwafanyia maendeleo wamachinga wa mkoa huo.

Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Augustino akizungumza na wandishi wa habari na machinga ambao waliojitokeza katika ofisi za chama mkoani hapa kumpongeza Rais Dk John Magufuli kwa kuwajali machinga.


Charles James, Michuzi TV

WAJASIRIAMALI wadogowadogo Jijini Dodoma (Wamachinga) wameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wDkt John Pombe Magufuli kwa kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zote ambazo zilikuwa zikiwakabili .

Akizungumza leo katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Dodoma Bruna Mponzi ambaye ni Mwenyekiti Msaidizi wa machinga Mkoani hapa amesema wameona ni vyema kurudisha fadhila kwa serikali kwa kila kitu walichofanyiwa kwani kazi zao kwa sasa wamekuwa wakifanya kwa uhuru mkubwa tofauti na hapo awali.

‘’ Kwa upande wetu mmekuwa watetezi wetu wa nguvu kwa sababu ni tofauti na awamu nyingine zilizopita tulikuwa tunaishi kwa shida na hofu kwenye maeneo yetu ya kazi lakini sasa tunaishi kwa uhuru mkubwa Zaidi’' Amesema Mponzi.

Naye Mweka Hazina wa Machinga Athuman Ally amesema wametafuta fursa hiyo kwa muda mrefu ya kumshukuru na kumpongeza Rais Magufuli kwa yale ambayo amewafanyia wamachinga katika jiji la Dodoma.

‘’ Mpaka sasa hivi tuna imani na Mh. Rais kwamba anaweza na ataendelea kutenda juu ya machinga zaidi ya hayo na anaweza kutoa tamko jingine zuri juu ya uhuru wa wamachinga''Amesema

Katibu wa Wamachinga Stendi ya Mabasi Dodoma Shaban Suleiman Kisamvu amesema, ‘’nimesimama hapa kuwakilisha salamu za wamachinga wa stendi ya mabasi wanamshukuru sana Rais Magufuli kwa kuweka stendi hiyo ambayo imekuwa ni ya kisasa zaidi’’ Amesema

Elizabeth Siame ni Mwenyekiti wa Wamachinga Soko la Sabasaba amesema anamshukukuru kwa kila kitu kwani kazi zao sasa zimekuwa zikifanyika kwa uhuru mkubwa huku Leonatha Ernest Msakafu amesema kwa kipindi cha nyuma wajasiriamali wadogo walikuwa wakihangaishwa ,wakinyanyasika lakini kwa sasa hawakumbani na changamoto yoyote ile huku

Katibu Mwezi wa CCM Mkoa wa Dodoma Henry Msunga Mwengi amesema wamachinga ni sehemu ya watanzania wanahaki kama watu wengine na wanastahili heshima.

‘’Kwa yote yalifanyika kwa sasa wamachinga wanapata heshima mno unajua kwanini kwasababu leo mmachinga anaheshimika leo machinga anaona fahari kwa kazi anayoifanya kwa kujitambulisha kuwa ni machinga.’’Amesema

Pili Agustino Mbanga ni katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma amewashukuru wamachinga wote mkoani hapa kwa kuthamini kwazi kubwa aliyoifanya Rais Magufuli .

‘’ kwakweli nyinyi wamachinga ni watu wema sana mmetambua fadhila alizowafanyia Rais Magufuli na ujumbe huu utafika kwa Mh. Rais ''Amesema Pili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...