Na Emmanuel Masaka, Michuzi TV
WAPINZANI zaidi ya wapinzani 50 katika Kata ya Dondo iliyopo Tarafa ya Kisiju wilayani Mkuranga mkoani Pwani wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) ili kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Chama hicho. 

Wanachama hao wapatao 54 wametoka katika vyama viwili vya upinzani ambavyo ni CUF na CHADEMA ambapo wameamua kurejesha kadi za vyama vyao na kupatiwa kadi za CCM wakati wa mikutano ya kampeni za mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga Mkuranga,Abdallah Ulega katika vijiji Vitatu vya Kata ya Dondo ambavyo ni Kibewa, Mpafu na Sotele 

Akiwapokea wanachama hao wapya, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkuranga Mzee Ally Msikamo amewataka wana CCM katika Kata hiyo kutoa ushirikiano kwa kuwasadia kuendana na sera za Chama hicho.

Kwa upande wake Ulega amewashukuru wanachama hao wapya kwa kutambua ukweli na kujiunga na CCM na kutoa mwito kwa wananchi wote kukichagua Chama hicho ili kishinde kwa kishindo 

Aidha akiwa katika kijiji cha Sotele Mgombea Ulega amewaahidi wanancha wa Kijiji hicho kuwatafutia mradi mkubwa wa maji ambao utamaliza kabisa kero hiyo.

Ulega amesema alikwishashughulikia kero hiyo kwa sehemu lakini iwapo wananchi watapigia kura CCM ikapata ushindi Oktoba 28 mwaka huu tatizo hilo linakwenda kuwa historia.

Katika hatua nyingine mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga ambaye ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amewaahidi vijana wa Kata ya Dondo tarafa ya kisiju Mashine ya kuendeshea Boti isaidie kuvusha watu kwenye kisiwa kidogo cha Dendeni iwapo atashinda kwenye Uchaguzi Mkuu.

Amesema yeye atakabidhi mashine hiyo lakini amewataka vijana hao kuwa wabunifu kwa kutengeneza boti yenyewe ili iwasaidie katika jitihada mbali mbali za maedeleo sambamba na kuvusha watoto kwenda na kurudi shule.Aidha amewataadharisha vijana hao kutumia mashine katika matumizi yaliyokusudiwa ili wajipatie kipato na wasiuze.

Hata hivyo Ulega amewaahidi wananchi wa kijiji cha Kibewa iwapo atashinda katika uchaguzi mkuu ataendelea kusimamia matengenezo ya barabara katika kijiji hicho, ipitike kipindi chote ili kuwapunguzia changamoto wananchi hao zitokanazo na barabara.
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega  akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi leo  Kata ya  Dondo.(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv)





Wanachama mpya 54 wakipokea Kadi za CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga, Ali Msikamo akizungumza baada  ya kuwapokea wanachama 54  kotoka vyema mabilimbali vya Upinzani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...