Charles James, Michuzi TV

IKIWA ni dakika za lala salama za kampeni za Uchaguzi Mkuu, Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile amefika katika kata ya Kingale wilayani Kondoa na kufanya mkutano wa kukiombea kura Chama cha Mapinduzi ili kipewe ridhaa ya kuongoza tena kwa kipindi cha miaka mitano.

Akizungumza katika kata hiyo, Ditopile amewaomba wananchi wa kata hiyo kuchagua mafiga matatu ya uongozi kwa maana ya Rais Dk John Magufuli, Mbunge Ally Makoa na Diwani Abushehe.

Ditopile amesema kwa kipindi cha miaka mitano serikali ya CCM ikiongozwa na Dk Magufuli imefanya mambo makubwa ya kimaendeleo katika sekta huku kila kata, jimbo na ngazi ya Taifa vikiguswa na kasi ya Dk Magufuli.

Amesema kwenye sekta ya nishati ya umeme, Rais Magufuli amefanya mageuzi makubwa ambapo umeme Umefika kila kijiji ikiwemo vijiji vya kata ya Kingale lakini pia amefanya maboresho makubwa kwenye sekta ya afya, elimu, miundombinu ya barabara.

" Dk Magufuli amefanya mageuzi makubwa kwenye nishati ya umeme leo kila kijiji kina umeme nchini nzima na hapa kwenu pakiwemo, ameboresha sekta ya afya kwa kujenga zaidi ya vituo 480 vya afya na kata ya Kingale hapa mlipata, kwenye vijiji sita vya kata hii mmepata Zahanati mbili na niwaahidi nitakuja hapa tushirikiane tujenge Zahanati nyingine ya tatu.

Hatujawahi kuona kiongozi wa kidini anatangaza hadharani kuunga mkono chama cha siasa, leo eti mtu anajiita sheikh anatangaza kuwa waislamu wanaiunga mkono Chadema ambacho kimechukua pesa za mabeberu ili kiunge mkono ushoga, hatuwezi kukubali kuona mtu mmoja anaharibu taswira ya Dini zetu, tumkemee na tumkatae kwa nguvu zote," Amesema Ditopile.

Amesema kwa kazi kubwa iliyofanywa na Dk Magufuli kwenye Jimbo la Kondoa Mjini na Kata hiyo ya Kingale itakua ni dhambi kubwa kumnyima kura za kishindo na kuwapigia wapinzani ambao kila siku wamekua wakihubiri machafuko, udini na ukabila jambo ambalo ni hatari kwa maslahi ya Nchi.

Mgombea huyo wa Ubunge leo ataendelea na ziara yake katika Jimbo la Chemba mkoani Dodoma ikiwa ni muendelezo wake wa kupita kila Jimbo ndani ya mkoa huu kukiombea kura Chama chake.

Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile (kulia) akizungumza na wananchi wa kata ya Kingale wilayani Kondoa alipoenda kukiombea kura Chama chake kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28.
Mgeni rasmi katika kampeni za CCM kata ya Kingale, Kondoa, Mariam Ditopile (kulia) akimnadi mgombea Udiwani wa kata hiyo, Abushehe pamoja na kumuombea kura Mgombea Urais, Dk John Magufuli na Mgombea Ubunge Jimbo la Kondoa Mjini, Ally Makoa.
Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile akizungumza na wananchi wa kata ya Kingale wilayani Kondoa alipoenda kuomba kura za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28 mwaka huu.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...