Wakazi wa wilaya ya Ludewa wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upigaji kura litakalofanyika siku ya kesho nchi nzima.

Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Ludewa mjini katika uwanja wa halmashauri Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema wananchi hawapaswi kuwapa nafasi watu wanaotaka kufanya majaribio katika uongozi.

Aliongeza kuwa Chama Cha mapinduzi kimeleta maendeleo na kimekwisha weka mikakati mbalimbali itakayoifanya nchi kuwa na Maendeleo zaidi.

Aidha katika mkutano huo walikuwepo waliokuwa viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa ngazi ya mkoa waliwataka wananchi kutopigia kura upinzani kwani wao walikuwa viongozi wanafahamu yanayofanyika.

 Fakiru Landala ambaye alikuwa mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Njombe amesema alifanya maamuzi ya kukihama Chama hicho kutokana na kuona CCM inapangua hoja zao kwa vitendo.
 
"Wakati nipo upinzani tulikuwa tunaangalia palipo na udhaifu wa maendeleo ndio fimbo ya kuwachapia CCM, lakini rais Magufuli amepangua hoja hizo kwa vitendo tumekosa chakukusema". Alisema

Naye aliyekuwa katibu wa CHADEMA  mkoani Njombe Alatanga Nyagawa aliwaambia wananchi kuwa viongozi wa CHADEMA wanawajua vyema kuwa hawana mipango endelevu juu ya kuiongoza nchi.

Alisema viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho wanawatumia wananchi kama daraja la kujipatia mafanikio binafsi.

"Wananchi hampaswi kudanganyika na wapinzani kwani sisi tulikuwa viongozi  tunayajua mambo yote yanayoendelea ndani ya CHADEMA hivyo mnapaswa kutusikiliza haya tunayo waambia. Alisema Nyagawa.

Awali mbunge huyo alifanya kampeni katika kata zote 26 za wilaya hiyo pamoja na vijiji 77 ambako alipita kumuombea kura rais John Pombe Magufuli na madiwani wa kata 11 zilizo na upinzani.

Baadhi ya wananchi wakifika kwenye mkutano wa kufunga kampeni wilayani Ludewa mkoani Njombe wakipunga mikono kwa mbunge mteule wa jimbo hilo Joseph (Hayupo pichani) Kamonga alipokuwa akihutubia.

Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya kampeni wilayani humo.
Aliyekuwa katibu wa CHADEMA mkoa wa Njombe Alatanga Nyagawa akiongea na wananchi ( hawapo pichani)
Aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Njombe Fakiru Landala akiongea na wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni wilayani Ludewa mkoani Njombe.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akijadiliana jambo na mgombea udiwani wa kata ya Ludewa.
Vijana wa CCM wilayani Ludewa wakiserebuka wakati wa mkutano wa kufunga kampeni wilayani humo.
 Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume akiwaapisha wanachama wa upinzani waliohamia CCM (hawapo pichani) anayefuata ni Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga na Mgombea udiwani wa kata ya Ludewa Monica Mchiro.

Waliokuwa Wanachama wa CHADEMA wakiwa wamepanga mstari tayari kwa kupewa kadi za kuhamia  CCM

Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume akiongea na wananchi wakati wa mkutano wa kufunga kampeni wilayani humo.
Baadhi ya wanakamati wa  timu ya kampeni CCM wilaya ya Ludewa wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Edna Haule, Felix Haule, John Kiula pamoja na Stella Ngairo.
 Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwapigia makofi wana kikundi cha ngoma ya mganda wakati kikitumbuiza walipokuwa wakifunga kampeni wilayani humo.

Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akimpa kadi ya CCM mmoja wa wanachama wa CHADEMA waliohamia CCM

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...