KATIBU Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof Elisante Ole Gabriel amewaeleza wanafunzi wa Chuo cha Serikali za Mitaa- Hombolo kuwa wao ni Viongozi watarajiwa hivyo wanawajibu wa kuhakikisha watakapokuwa viongozi wanakidhi matarajio ya wale watakaokuja kuwaongoza.

Prof Gabriel ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada iliyohusu nafasi ya viongozi wa kuchaguliwa katika kuleta maendeleo kwa jamii anayoiongoza kwenye hafla ya kuwatunuku zawadi wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao na wafanyakazi bora wa chuo cha Hombolo iliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Dodoma Novemba 25, 2020.

Amesema katika kipindi hiki ambacho nchi ya Tanzania imeingia katika uchumi wa kati viongozi wanawajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba wanakidhi matarajio ya Watanzania.

Prof Gabriel ameongeza kuwa nchi nyingi na taasisi zimekuwa zikikwama kufikia malengo tarajiwa kwa sababu ya kukosa usimamizi mzuri.

“ Kuwa na rasilimali ni jambo moja, lakini kusimamia rasilimali hizo ni jambo la muhimu zaidi, taasisi nyingi zimekwama kwa kushindwa kusimamia rasilimali zake ikiwemo rasilimali watu, rasilimali fedha na rasilimali miundombinu,” amesema Prof. Gabriel.

Kwa mantiki hiyo ameupongeza Uongozi wa Chuo cha Hombolo kwa kusimamia agenda ya uongozi huku akisema kuwa elimu hiyo wanayoitoa kwa wanafunzi wa chuo hicho itawasaidia wanafunzi hapo mbeleni watakapokuwa viongozi.

Ameendelea kusema kuwa kiongozi yeyote wa kuchaguliwa au kuteuliwa ili awe kiongozi bora ni muhimu kuzingatia mambo matatu ambayo ni kufahamu hasa anaowaongoza wana mahitaji gani pia Kiongozi atambue kuwa hatakumbukwa kwa cheo chake bali kwa mchango wake kwa jamii ile anayoiongoza na tatu, awe mtu anayewashirikisha wale anaowaongoza katika kutatua changamoto zao.

“Washirikishe wale unaowaongoza na ndipo utakapoweza kutatua changamoto, kiongozi mzuri ni yule anayeziona changamoto na kuzibadilisha kuwa fursa, na kwa kufanya hivyo ndipo utaweza kukidhi matarajio ya wale unaowaongoza,” Amesisitiza Prof. Gabriel.

Katika hafla hiyo ya 12 ya chuo hicho, Prof  Ole Gabriel alikuwa Mtoa mada maalum na aliwasilisha mada hiyo ya nafasi ya viongozi wa kuchaguliwa na wakuteuliwa katika kuleta maendeleo kwa jamii ili kuwakumbusha wajibu wao mkubwa kwa jamii.

Sehemu ya Wanafunzi na Wafanyakazi wa Chuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo waliohudhuria hafla ya kutunukiwa zawadi wafanyakazi na wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo iliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Dodoma Novemba 25,  2020.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha mada katika hafla ya kutunukiwa zawadi Wafanyakazi na Wanafunzi waliofanya vizuri wa Chuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo iliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Dodoma Novemba 25, 2020.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiwasalimia Wanafunzi na Wafanyakazi wa Chuo cha Serikali za Mitaa- Hombolo (hawapo pichani) alipokuwa akitambulishwa katika hafla ya kutunukiwa zawadi wafanyakazi na wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo iliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Dodoma Novemba 25, 2020.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia), akifurahia jambo alipokuwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli (kushoto)  walipokutana kwenye Hafla ya Kutunukiwa zawadi wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo cha Serikali za Mitaa- Hombolo waliofanya vizuri katika masomo.  Prof. Elisante Ole Gabriel  alikuwa Mtoa mada maalum katika hafla hiyo iliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Dodoma Novemba 25, 2020.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...