Na Rosena Suka IJA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare ametoa pongezi kwa Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kuwa kinara katika kutoa mafunzo ya njia za utatuzi mbadala wa migororo ya ardhi mkoani humo. Pongezi hizo alizitoa alipokuwa anafunga mafunzo Novemba, 27 mwaka huu kwa washiriki thelathini na tatu wakiwemo wanaotoka katika Mabaraza ya Kata, Kijiji na Jumuiya Maridhiano ya usuluhishi wa migogoro ya Ardhi. 

Mafunzo haya yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Kilombero katika mji wa Ifakara.  Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kimepewa jukumu la kuendesha mafunzo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani  (FAO) likishirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia mradi wake unaojulikana kama Msaada wa Kuimarisha Usimamizi wa Miliki kwa Uwajibikaji katika Ardhi, maeneo ya uvuvi na misitu.

Mafunzo haya yamekuwa ni mwendelezo wa mafunzo ya aina hiyo ambayo yalielekezwa kutolewa katika wilaya za mkoa wa Morogoro. Mpaka sasa wilaya za Mvomero, Kilosa  na Kilombero zimeshapata mafunzo hayo. Wilaya ya Ulanga pia inatarajiwa kupata mafunzo hayo hivi karibuni.

Akiongea katika hafla hiyo Bwana Sanare alisisitiza kwamba mafunzo haya yasiishie tu kwa wajumbe wa Mabaraza ya Usuluhishi.  Ameomba mafunzo yaende mbali zaidi, kwa viongozi mbalimbali waliopo mkoani na Halmashauri na ameshauri viongozi wa vijiji pia wapate mafunzo. Katika kusisitiza hilo Mkuu wa mkoa alitoa wito kwa wakuu wa halmashauri zote za Mkoa zitenge bajeti kwa ajili ya mafunzo haya muhimu.

Kwa upande wake Ndugu Justus Mulokozi, Mratibu wa mafunzo amesema ni vema viongozi wa mabaraza ya ardhi katika kata na vijiji hasa upande wa migogoro ya ardhi wanaposuluhisha migogoro wakatafuta chimbuko la migogoro na kuhakikisha katika usuluhishaji  madalali hawahusiki na badala yake migogoro hiyo ihusishe wahusika wa suala hilo pekee.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare akiwa na viongozi wengine wakati wa kufunga  mafunzo ya njia za utatuzi mbadala wa migororo ya ardhi kwa washiriki thelathini na tatu wakiwemo wanaotoka katika Mabaraza ya Kata, Kijiji na Jumuiya Maridhiano ya usuluhishi wa migogoro ya Ardhi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare(kulia) akimkabidhi Mshiriki wa Mafunzo cheti hake  mara baada ya kuhitimu mafunzo ya njia za utatuzi mbadala wa migororo ya ardhi kwa washiriki thelathini na tatu wakiwemo wanaotoka katika Mabaraza ya Kata, Kijiji na Jumuiya Maridhiano ya usuluhishi wa migogoro ya Ardhi.
Baadhi wa washiriki wa  mafunzo ya njia za utatuzi mbadala wa migororo ya ardhi wakiwa katika picha ya Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro mara baada ya kuhitimu mafunzo ya njia za utatuzi mbadala wa migororo ya ardhi kwa washiriki thelathini na tatu wakiwemo wanaotoka katika Mabaraza ya Kata, Kijiji na Jumuiya Maridhiano ya usuluhishi wa migogoro ya Ardhi.
Picha ya Pamoja ya baadhi ya washiriki na wahadhiri kutoka chuo cha uongozi wa mahakama Lushoto mara baada ya mafunzo ya njia za utatuzi mbadala wa migororo ya ardhi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...