Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya,akizungumza  wakati wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira,akiongea kwenye kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma.

Mrajis wa vyama vya ushirika Dk Benson Ndiege,akiwasisitiza jambo washiriki wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya KCBL, Dk Gervas Machimu,akizungumza wakati wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma.

 Mwenyekiti wa Kilimanjaro Co-operative Bank Limited  (KCBL), Balozi Ibrahim,akitoa maelezo kwa washiriki wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma.

Afisa Mkuu wa biashara wa CRDB, Dk. Joseph Witts,akizungumza wakati wa  kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma

 

Baadhi ya washiriki wa  kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald  Kusaya,akiteta jambo na Mrajis wa vyama vya ushirika Dk Benson Ndiege wakati wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma


=====  =========  ========
SERIKALI imewataka watu wote waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha na kurudisha mali hizo kwa hiari kabla ya kuchukuliwa hatua za Kisheria.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald  Kusaya  wakati wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL).

 Kusaya amesema kuwa  mali zote za vyama vya ushirika zilizochukuliwa bila kufuata utaratibu zitarudi kwenye mikono ya serikali.

Aidha,amebainisha kuwa wamefanikiwa kurejesha mikononi mwa  serikali mali 59 za ushirika zilizochukuliwa bila kufuata utaratibu kuna viwanja,, majumba, mitambo na vingine vyote vina thamani ya bilioni 68.9 na zoezi ni endelevu.

“Kama kuna mtu ana mali za ushirika kwa njia zisizo sahihi azirudishe kwa hiari bila hivyo tuna nguvu nyingi za ziada haijalishi zipo wapi lazima tutazipata,” amesema Kusaya.

Kusaya ameendelea kubainisha kuwq serikali itakuwa bega kwa bega na benki hiyo ua ushirika ya Kilimanjaro ili kuhakikisha inazaa matunda kwa manufaa ya Watanzania.

“Kama tunaamini katika ushirika lazima tuuheshimu  na kulenga kufanya ushirika wa kibiashara katika kumkomboa Mtanzania tunataka kila mwanaushirika awe bilionea,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya KCBL, Dk Gervas Machimu amesema benki hiyo iko imara kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt.Machimu amesema kuwa wameweza kushirikiana na Benki ya CRDB na wana bodi ya pamoja kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.

Hata hivyo ameelezea kuwa Serikali inayo ndoto ya kuendeleza viwanda katika nchi na kutoa huduma katika kilimo na biashara na uwepo wa benki hiyo utasaidia kuendeleza  sekta za uzalishaji na kusaidia zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanaotegemea kilimo kunufaika.

Naye Mrajis wa vyama vya ushirika Dk Benson Ndiege amesema kuwa KCLB ni chama cha ushirika kilichoandikishwa kama benki na kimepata leseni ya kuhudumu kama benki ya ushirika kwa wananchi wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga katika kilimo cha kahawa.

Amebainisha kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo, ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na benki ya CRDB wamefanya kila liwezekanalo ili benki isimame na kuhudumia makundi mbalimbali kama wakulima, wafugaji, wavuvi, wajasiriamali, wafugaji.

“Kama tukiamua leo kuikuza benki hii kwa kununua hisa tunaweza kuifikisha mbali, vyama vikuu vya ushirika viko 46  lakini vinavyofanya kazi vizuri viko 30,” amesema

Amesema benki ya ushirika ya Kenya inafanya vizuri kutokana na uwezezaji uliofanyika na Tanzania ikiamua jambo hilo hakuna linaloshindikana.

“Kama tukifanya mabadiliko kwenye sekta ya kilimo, viwanda na uvuvi kama walivyofanya Kenya na kwenye benki ya ushirika wana uwekezaji ndio maana wamefanikiwa na benki yao ni ya tatu kwa ukubwa Kenya,” amesisitiza Dk.Ndiege

 Mwenyekiti wa Kilimanjaro Co-operative Bank Limited  (KCBL), Balozi Ibrahim amevitaka vyama vya ushirika kuchangamkia fursa ya uwekezaji kwenye vyama hivyo.

Amesema  wanachama wengi wa KDF wamewekeza kwenye benki hiyo.

Ofisa Mkuu wa biashara wa CRDB, Dk. Joseph Witts amesema  kuwa CRDB iliundwa na ushirika na baadaye kuwa benki ya biashara.

Amesema wana kitengo cha kutoa mikopo kwa wakulima na wazalishaji mbalimbali.

“Mikopo yote tunayoitoa kwenye kwenye vyama vya ushirika   inalipwa vizuri,” alisema

Amebainisha wametoa bilioni saba kama mtaji kwenye benki ya KCBL.

Amesema CRDB ina menejimenti ndani ya benki hiyo na  wajumbe wa bodi ya CRDB wengine wako kwenye benki ya KCBL ili kuweza kuborsha utendaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...