Wanafunzi wa Kitanzania kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamefanikiwa kuwa miongoni mwa vinara wa Fainali za Shindano la Dunia la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano la Huawei lililofanyika mwishoni mwa wiki.

 

Timu ya wanafunzi hao kutoka Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (COICT) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, walifanikiwa kufika hatua hiyo ya mashindano kufuatia kuibuka vinara katika Mashindano hayo miongoni ya mwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

 

Shindano hilo linalenga kutoa jukwaa kwa vijana wenye vipaji kwenye TEHAMA kuonyesha uwezo wao, kushindana na kuwasiliana, kuhimiza utafiti wa TEHAMA, na kusaidia ukuaji wa mfumo thabiti wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

 

Licha ya kuwa washiriki wapya zaidi wa Mashindano ya hayo tangu walipoanza kushirikia mwaka 2017, wanafunzi wa Kitanzania wamekuwa wakifanya vizuri zaidi katika mashindano hayo. Mnamo 2019, ni timu tano tu za Kiafrika ikiwemo Tanzania zilizofanikiwa kuingia fainali hizo ambapo zilifanikiwa kuvuna tuzo moja kati ya tatu, ikilinganishwa na timu 13 mwaka huu, ambazo zimeshinda medali saba.

 

Timu ya wanafunzi hao kutoka watanzania iliundwa na wanafunzi Mpoki Abel Mwaisela, Hongo Kelvin, Henry Kihanga, Aghatus Biro, John Lazaro na Elisante Akaro.

 

Akizungumzia ushindi huo kwa niaba ya wenzake, mwanafunzi Kelvin Hongo kutoka Tanzania alisema: "Mashindano hayo ya Huawei pamoja na kuwajenga kiuwezo yamekuwa na tija kwao ikiwemo kuwapatia vyeti vya utambuzi kuhusu mafanikio yao katika taaluma hiyo,’’.

 

Mafanikio ya wanafunzi hao yanatajwa kuwa ni kwa sababu ya kutambuliwa kwa jitihada za nchi za Afrika katika kujenga vipaji vipya kwenye sekta ya TEHAMA ambao watakuwa kichocheo katika kurejesha ustawi wa bara hili baada ya janga la COVID 19.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Huawei imesaini makubaliano ya ushirikiano na Vyuo vikuu zaidi ya 10 vya Tanzania juu ya kuanzisha Taaluma za TEHAMA za Huawei. Ushirikiano huu umewezesha zaidi ya 600 kutoka Vyuo vikuu kupata Vyeti vya TEHAMA  vya Huawei, ambayo huwafanya wawe washindani bora kwenye ajira zinazohusisha TEHAMA.

 

Profesa William Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliwasifu wanafunzi hao kwa ushindi wao mkubwa na kuinua uwakilishi wa Chuo hicho.

“Nawapongeza wanafunzi kwa ushindi. Huu ni ushahidi dhahiri wa ubora wa masomo kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambacho huwaandaa wanafunzi wake kuwa wabunifu katika sayansi na teknolojia. Chuo Kikuu kinathamini ushirikiano na Huawei katika kuziba pengo la maarifa ya TEHAMA kwa wanafunzi wetu, na nachukua fursa hii kuwahimiza sana wanafunzi wote kushiriki katika programu za Huawei ''. Alisema Profesa Anangisye.

Kwa upande wake, Bwana Hou Tao, Makamu wa Rais wa Huawei Ulimwenguni, aliangazia shauku ya kuvutia ya wanafunzi, ambayo inahitajika sana kwa ujumuishaji wa dijiti wa Afrika katika zama ambazo mvuto wa ujuzi wa mahali pa kazi tayari unabadilika mtandaoni.

 "Kama kampuni ya kibinafsi inayohudumia soko la Kiafrika kwa zaidi ya miaka 20, Huawei imejitolea na itabaki kuwa mshirika wa kuaminika wa serikali na taaluma katika kujenga ushindani wa talanta ya TEHAMA ya ushindani, kuimarisha ujengaji uwezo na kuongeza uwezo wa watu kidigitali," alisema Bw. Hou.

Mashindano ya TEHAMA ya Huawei mwaka huu yalivutia takribani wanafunzi 150,000 kutoka vyuo vikuu zaidi ya 2,000 katika nchi zaidi ya 82. Wanafunzi 327 kutoka nchi 39 walishiriki fainali hizo zilizofanyika kwa njia ya mtandaoi, na kufanya kiwango kuwa kikubwa zaidi kwa miaka yote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...