MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imekuwa mshindi wa pili ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) katika kipengele cha Mamlaka za maji.

Tuzo hizo zinatolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) zimefanyika jana  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Fedha wa DAWASA CPA Sais Kyejo amesema imekuwa ni mara ya kwanza kushiriki katika tuzo hizo na wamefanikiwa kushika kwenye nafasi ya pili.

Kyejo amesema, kushika kwa nafasi hiyo kunaonesha wahasibu wanajua  kazi wanayofanya na wanazingatia viwango.

"Kupata kwa tuzo hii kuna maana kubwa sana kwa taasisi yetu sambamba na wahasibu waliopo kwenye idara ya fedha," amesema Amesema, wanahaahidi kuendelea  kuwa katika Viwango bora kila siku kwani kupata kwa tuzo hiyo kumeleta chachu kwenye taasisi na idara nzima.


"Tumeshiriki kwa mara ya kwanza, na tumeweza kufanya vizuri na hili linaleta chachu katika taasisi yetu na idara nzima,"

Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja aliweza kupokea tuzo hiyo ya mshindi wa pili ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) katika kipengele cha Mamlaka za maji.
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja akipokea tuzo kutoka kwa mgeni rasmi Kamishna anayesimamia Sekta Ndogo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamaja ya mshindi wa pili ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) katika kipengele cha Mamlaka za maji.
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja akipongezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Isaya Jairo mara baada ya kupokea tuzo ya mshindi wa pili ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) katika kipengele cha Mamlaka za maji.
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja(katikati) akiwa na maofisa wa DAWASA wakati wa utoaji wa tuzo za uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) zinatolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).
Mkurugenzi wa Fedha wa DAWASA CPA Sais Kyejo(wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa DAWASA wakati wa utoaji wa tuzo za uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards)zinatolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).
Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam ( DAWASA). CPA Sais Kyejo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mamlaka hiyo kushinda tuzo ya mshindi wa pili ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) katika kipengele cha Mamlaka za maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...