Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),  kimeibuka mshindi wa pili ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) katika kipengele cha Vyuo vya elimu ya juu.

Tuzo hizo zinatolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)  zilizofanyika jana  jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo Kamishna anayesimamia Sekta Ndogo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamaja ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kuwa Tuzo hizi zina maana kubwa sana kwa Taasis na kwa Wahasibu ili kuweza kujipima kama tunaweza kuendana na viwango vya Kimataifa vya uandaaji wa hesabu na itawasaidia kuhakikisha kwamba wanaendelea kudumisha viwango vya huduma zao. 
 
Pia amezipongeza Taasis zote zilizoshiriki katika tuzo hizo kwani kufanya hivyo ni kipimo tosha cha uwajibikaji. 
 
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzidi hiyo Afisa Fedha Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Bw. Peter Lubuwa amesema hii ni mara ya pili kwa SUA kushiriki katika hizo ambapo mwaka jana walikuwa washindi wa tatu.

“Tumekuwa washindi wa pili Mwaka huu tofauti na mwaka jana ambapo tulikuwa washindi wa tatu hivyo tunaamini Mwakani tutakuwa wa kwanza” alisema Bw. Peter
Mgeni rasmi Kamishna anayesimamia Sekta Ndogo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamaja akimkabidhi tuzo Kaimu Mkuu Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Peter Lubuwa ya mshindi wa pili ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) katika kipengele cha kipengele cha Vyuo vya elimu ya juu.
Mgeni rasmi Kamishna anayesimamia Sekta Ndogo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamaja akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa pili wa tuzo za uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019(Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) zinayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...