Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Innocent Bashungwa Aliyesimama Akiwashuhudia Rais wa TFF Wales Karia Kushoto na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Eliamani Sedoyeka Kulia Akishuhudia utiwaji wa  Saini Makubaliano ya Ushirikiano Kati ya Shirikisho la Soka TFF na  Chuo cha Uhasibu Arusha Leo Januari 27 Jijini Arusha.

Rais wa TFF Wales Karia Kushoto na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Eliamani Sedoyeka Kulia Wakionesha Mkataba wa Ushirikiano Waliosaini Kuendeleza Mchezo wa Soka Baina ya Taasisi Hizo Leo Januari 27 Jijini Arusha.

 

Mkuu wa  Chuo cha  Uhasibu  Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka (wa tatiu kulia) Akitoa Maelezo kwa  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Innocent Bashungwa alipotembelea ,maeneo mbalimbali ya Chuo Hicho Leo Januari 27 Jijini Arusha.

Baadhi ya Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo cha  Uhasibu  Arusha (IAA) Wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Innocent Bashungwa (Hayupo Pichani) alipokuwa Akitoa Hutuba baada ya Kushuhudia Utiwaji Saini Makubaliano ya Ushirikiano Kati ya Shirikisho la Soka TFF na  Chuo cha Uhjasibu Arusha Leo Januari 27 Jijini Arusha.

Baadhi ya Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo cha  Uhasibu  Arusha (IAA) Wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Innocent Bashungwa Alipokuwa Akitoa Hutuba baada ya Kushuhudia Utiwaji Saini Makubaliano ya Ushirikiano Kati ya Shirikisho la Soka TFF na  Chuo cha Uhjasibu Arusha Leo Januari 27 Jijini Arusha.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Innocent Bashungwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chuo cha  Uhasibu  Arusha (IAA) Pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Mara Baada ya Kusaini Makubaliano ya ushirikiano Katika Kundeleza Soka Nchini leo Januari 27 Jijini Arusha.

……………………………………………………………………………

Na: Eleuteri Mangi- WHUSM, Arusha.

Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kimesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Shirikisho la Soka nchini (TFF) ili kuendelea kukuza michezo nchini.

Akizunzungumza mara baada ya utiwaji wa saini makubaliano hayo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amepongeza hatua hiyo ya Chuo cha Uhasibu Arusha kuunganisha taaluma na sekta ya michezo hatua inayosaidia kulea, kukuza na kuendeleza vipaji katika michezo mbalimbali.

“Tutakitumia chuo hiki kama mfano kwa kufanikiwa kuunganisha mnyororo wa thamani kati ya taaluma na michezo, hatua hii ni mfano wa kuigwa na vyuo vingine nchini ili kiuandaa wanataaliuma na wanamichezo ambao wataleta tija kwa taifa kwa kujiongezea vipato vyao na pato la taifa” alisema waziri Bashungwa.

Awali akiongea katika hafla hiyo fupi ya utiwaji wa saini ya makubaliano hayo Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Eliamani Sedoyeka alisema hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuendeleza mitaala ya michezo hususan somo la uongozi wa soka kwa ngazi ya Cheti, Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili na hatimae hatiua ambayo itasaidia katika uanzishaji na uendeshaji wa shule ya uongozi wa soka.

“Mwaka ujao wa masomo wa 2021/2022, tumepanga kutoa ufadhili wa masomo kwa vijana watakaofanya vizuri katika soka, na TFF watatusaidia katika kuwapata vijana hao, chuo kitawapa ufadhiri wa masomo kwa upande wa ada na malazi” alisema Prof. Sedoyeka.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF Wales Karia alisema mkakati huo wa chuo cha Uhasibu Arusha ni jawabu la kusimamia na kuendeleza wanamichezo ambao walikuwa wanapotea baada ya kumaliza kidato cha nne au cha Sita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...