Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akipokea taarifa ya Changamoto ya tope iliyotokea Kunduchi jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mhadhiri wa Jiolojia wa Chuo Kikuu ch Dar es Salaam, Dk. Remigius Gama.
Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Jiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia na utafiti wa madini Tanzania  bwana Maruvuko Msechu akiwasilisha Taarifa ya ripoti ya changamoto ya Tope  iliyotokea Kunduchi Jijini Dar es Salaam Novemba mwaka jana.

Wajumbe wa kamati pamoja na watalamu waliohusika katika utafiti wa changamoto ya Tope iliyotokea Kunduchi Jijini Dar es Salaam Novemba mwaka jana.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amepokea ripoti  ya utafiti iliyofanywa na wataalamu wa Jiolojia kuhusiana na kuwepo kwa changamoto ya Tope katika eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam Novemba mwaka jana.

Mhe. Chongolo ampokea taarifa hiyo leo ofisini kwake kutoka kwa Timu ya wataalamu iliyokuwa inacunguza changamoto hiyo ikiongozwa na Mhadhiri wa Jiolojia kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk. Remigius Gamba, ambaye ndio kiongozi mkuu wa kamati hiyo.

Akizungumza mara baada ya kupokea kwa taarifa hiyo, Mhe. Chongolo ameeleza kuwa mara baada ya kutokea kwa changamoto hiyo, Serikali ilichukua hatua ya  kuunda kamati ya wataalamu kwa ajili ya kuchunguza hali hiyo na hivyo kuipongeza kutokana na kazi kubwa waliyoifanya.

Mhe. Chongolo ametaja watalamu waliohusika katika utafiti wa changamoto hiyo kuwa ni kutoka  Taasisi ya Jiolojia na utafiti wa madini Tanzania (AGST), Chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia shule ya migodi na madini idara ya Jiosayansi, Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) pamoja na  Chuo cha mafunzo ya Jiosayansi (AMGC.)

Ameongeza kuwa kupitia ripoti hiyo, ushauri uliotolewa na wataalamu hao utafayiwa kazi kwa pamoja kama Serikali kuanzia ngazi ya wilaya hadi ile ya juu inayohusiana na uchakataji wa taarifa pamoja na utekelezaji wake.

Hata hivyo Mhe.Chongolo amesema kuwa utafiti huo ulikuwa ukifanyika kwa kushirkiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Abuubakari Kunenge na kwamba kutokana na umuhimu huo ataiwasilisha kwakwe ili aweze kujua matokeo ya kamati hiyo.

Hata hivyo Mhe. Chongolo amewataka wananchi kuacha kusikiliza taarifa zisizo rasmi kutoka katika vyanzo mbalimbali na badala yake wasikilize na kufuata maelekezo yatakayotolewa na  Serikali kupitia watalaamu wake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...