Timu ya Mtwivila City (Ifuenga) wakishangila ushindi baada ya kutinga hatua ya fainali mara baada ya kuifunga timu ya Irole fc kwa jumla ya goli mbili moja.


mwenyekiti wa umoja wa vijina wa chama cha mapinduzi (CCM) Makala Mapessa akiwa na kocha wa timu ya Mtwivila City (Ifuenga) baada ya mechi ya nusu fainali na kuingia fainali
Mwenyekiti wa umoja wa vijina wa chama cha mapinduzi (CCM) Makala Mapessa akifuatilia mchezo wa nusu fainali ya ligi ya mkoa wa Iringa kati ya Ifuenga United na Irole fc uliochezwa katika chuo cha Mkwawa

 


Na Fredy mgunda,Iringa.

Mwenyekiti wa vijana wilaya ya Iringa vijijini amezipongeza timu zote zilizoshiriki ligi ya mpira wa miguu mkoa wa Iringa (Asas super league) kwa kuonesha uwezo mkubwa wa kuchezea kabumbu kwa kuwa na na wachezaji wengi wenye vipaji vya hali ya juu kwa ngazi ya mkoa hadi kimataifa.


Akizungumza mara baada ya mchezo baina ya Mtwivila city dhidi Irole Fc uliomalika kwa timu ya Ifuenga United kutinga hatua ya fainali mara baada ya kuwafunga timu ya Irole Fc kwa jumla ya goli mbili moja katika uwanja wa chuo kikuu kishiriki cha Mkwawa,mwenyekiti wa umoja wa vijina wa chama cha mapinduzi (CCM) Makala Mapessa alisema kuwa halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini imekuwa na timu bora kila mwaka ndio maana kila mwaka lazima kwenye nusu fainali au fainali kuwe na Timu inayotoka halmashauri hiyo.

Alisema kuwa umoja wa vijan wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa umekuwa ukitoa ushirikiano wa asilimia 100 kwa timu zote ambaozo zimekuwa zinashiriki mashindano yoyote yale kwa kujua thamani ya vipaji vya wachezaji wa mpira wa miguu katika wilaya hiyo.

Mapessa aliwapongeza wadau wote ambao wamekuwa wakisaidia kukuza vipaji na Timu zote za kutoka wilaya hiyo katika mashindano mbalimbali ambayo wamekuwa wakishiriki kwa namna moja au nyingine.

"Moja kati ya wilaya yenye vijana wenye vipaji mkoani Iringa ni wilaya ya Iringa vijijini ambayo imekuwa ikitoa timu nyingi bora kwenye mashindano mbalimbali mkoani Iringa"alisema

Akizungumzia fainali ya Asas super league alisema kuwa ubingwa wa ligi hiyo lazima ubaki katika timu ya Mtwivila city (Ifuenga) kwa kuwa timu hiyo inawachezaji wengi wazuri ambayo wanaweza kushinda na timu yoyote ile kutokana na ubora walio nao.

Mapessa alisema kuwa Mtwivila city (Ifuenga) inauwezo wa kuifunga timu yoyote ile ambayo itakuwa inashiriki mashindano au ligi ambayo timu hiyo inashiriki kwa ajili ya ubora ambao wachezaji wake wanao kwa sasa.

Alimazia kwa kuwataka viongozi wote kuhakikisha wanashinda ubingwa wa ligi ya mkoa wa Iringa (Asas super league) kwa namna yoyote ile kwa kuwa timu hiyo ina wachezaji wenye ubora na wanavipaji vya kushiriki mashindano mbalimbali mkoani Iringa na nje ya mkoa wa Iringa.

Ikumbukwe kuwa Bingwa wa ligi hiyo iliyojizoelea umaarufu nchini kutokana na udhamini wa kampuni ya maziwa ya Asas ataondoka na sh milioni 2.5 huku mshindi wa pili akichukua milioni 1.5 na mshindi wa tatu ataibuka na laki 750000 baada ya zawadi kuongezwa kwa washindi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...