Mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu
kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM wa kati kati akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wanawake wa Mkoa wa Pwani wakimshangilia
kwa furaha.


Na Victor Masangu, Pwani

MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kupitia tiketi ya Chama cha
mapinduzi Hawa Mchafu, amewahimiza wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari kuhakikisha kwamba wanajenga tabia ya kula matunda ambayo
yameoshwa na maji safi na salama  pamoja na kunawa mikono yao  kwa
lengo la kuweza kuthibiti hali ya mlipuko wa magonjwa mbali mbali
ambayo wanaweza kuyapata.

Mchafu aliyasema hayo wakati akizungumza kuhusiana na mikakati yake
aliyojiwekea katika  masuala  mbali mbali ya kuboresha sekta ya elimu
ambapo alibainisha kuwa wanafunzi wanapaswa kuwa ana afya njema wakati
wote hivyo wanatakiwa kuzingatia taratibu zote ambazo zinatolewa na
wataalamu wa afya ili kuepeukana na mlipuko wa magonjwa hayo.

“Kwa sasa hivi katika baadhi ya maeneo kuna shule ambazo zina miti ya
matunda mbali mbali hivyo wakati mwingine yanawez kuanguka chini na
baadhi ya wanafunzi waneweza kuyaokota na kula pasipo kuyaosha lakini
mimi nichukue fursa hii kuwaasa wawe na utaratibu wa kuosha mikono yao
pamoja na kuosha matunda hayo hii itasaidia zaidi katika kujikinga na
magonjwa,”alisema Mchafu.

Pia Mchafu aliongeza kuwa katika kuunga mkono juhudi za serikali
katika kupambana na mlipuko wa magonjwa mbali mbali atashirikiana bega
kwa began a walimu pamoja wataalamu wa afya ili waweze kutoa mafunzo
juu ya umuhimu wa kunawa mikono wakati wa kula pamoja na kuachana na
tabia ya kula matunda au vyakula ambayo hayijaoshwa.

Kadhalia aliongeza kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni
kuhakikisha kwamba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanasoma
katika mazingira ambayo ni rafiki na wakiwa katika afya nzuri hivyo ni
vema kukawa na mipango madhubuti katika suala zima ya usafi wa
mazingira katika maeneo mabali mbali hususan katika ulaji wa vyakula.

Katika hatua nyingine aliwakumbusha wanafunzi hao pia kuhakikisha
kwamba wanakunywa maji ambayo yamechemshwa ili kuondokana na kupata
magonjwa  mbali mbali ikiwemo kuumwa na matumbo na ambayo mengine
yanakuwa na uchafu ambao unaweza kupelekea kusababisha madhara makubwa ya kiafya.

Pia  Mbunge  mchafu  aliahidi kuendelea kushirikiana na wananchi
pamoja na wataalamu wa afya katika kuweka mipango madhubuti ya kutoa
elimu ya mara kwa mara hasa katika maeneo ya vijijini ili kuweza kutoa
elimu ambayoitaweza kuwa ni moja ya msaada na mkombozi mkubwa wa
kuwasaidia wananchi kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...