JESHI la polisi Mkoa wa Kinondoni linamshikilia mwanamke mmoja, Pendo Carlos, kwa tuhuma za kumuua mtoto wa mume wake na kujaribu kuwauwa watoto wengine wawili kwa kuwatumbukiza ndani ya shimo la kuvunia maji ya mvua.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha Polisi cha Osterbay jijiji Dar es Salaam, leo Januari 20,2021 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa polisi (ACP) Ramadhani Kingai amesema, tukio hilo limetokea  jana, Januari 19,2021 majira ya saa saba mchana huko Tegeta A .

Amesema jeshi la polisi lilipokea taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu aitwaye Roda Beda aliyewaeleza kuwa amepokea ujumbe kwa njia ya simu ya mkononi kutoka kwa mtuhumiwa ukisema kuwa "mdogo wangu nimeamua kujiua kwa sababu ya kunyanyaswa na wakwe zangu"

Amesema mtoa taarifa baada ya kupokea ujumbe akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliondoka na kuelekea nyumbani, ambapo alikuta mlango umefungwa na alipogonga geti ili afunguliwe hapakuwa na dalili za mtu kufungua.

Amesema alifanya jitihada na kufanikiwa kuvunja geti kisha akaingia ndani.

"Baada ya kuingia ndani alikuta mwili wa binti wa mume wa dada yake aitwaye Belinda Carlos (17) umelazwa chini na wakati akiendelea kuchunguza chanzo ndio aliposikia kelele za watoto wakilia ndani ya shimo la kuvunia maji ya mvua na ndipo akaomba msaada kwa wananchi na kufanikiwa kuwatoa watoto wawili Bertha (4) na Brighton (6) wakiwa hai kutokana na shimo hilo kuwa na Maji machache"amesema ACP Kingai

Akaendelea kueleza kuwa baada ya mtuhumiwa kufanya tukio hilo aliondoka na kuelekea Sinza ambapo alikodi chumba kwenye hoteli ya  Movec lodge chumba namba 111 na kunywa kitu kinachosadikika kuwa ni sumu kwa nia ya kutaka kujiua, lakini wahudumu walifanikiwa kumuokoa na kumpeleka hospitali ya Sinza palestina ambapo amelazwa akiwa chini ya ulinzi wa Polisi na hali yake ni mbaya" ameeleza ACP Kingai

Aidha Kingai amefafanua kuwa baada ya jeshi hilo kupata taarifa na kufika eneo la tukio na kubaini uwepo wa maiti ya binti aitwaye Brenda Carlos ,ambapo ulikuwa umelazwa chini ukiwa umefungwa mtandio shingoni kwa kukazwa mithilii ya kunyongwa.

"Chanzo cha tukio hili inasadikiwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia,inadaiwa kuwa mtuhumiwa ndie aliesababisha kifo cha mume wake Carlos Myakunga (52) aliyefariki mwezi Mei 2020 kwa maradhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...