Na Victor Masangu, Pwani

MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Gunini Kamba amewawatahadharisha na kuwaonya vikali  baadhi ya  wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  kuachana kabisa na vitendo vya kujisaidia  katika maeno ya vichaka kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha madhara makubwa ya  kutokea kwa mlipuko wa magonjwa mbalimbali ikiwemo kipindu pindu.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na   mikakati waliyojiwekea katika ngazi ya Mkoa katika kupambana na kudhibiti kabisa hali ya kuwepo kwa magonjwa ya mlupiko katika maeneo mbalimbali hususani katika mkusanyiko wa watu wengine kama vile mashuleni.

“Kwa sasa hivi tupo katika msimu mpya wa mwaka wa 2021 ambapo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari tayari wamefungua shule zao na kuanza masomo lakini pamoja na mambo mengine yote ni lazima sisi kama wataalamu wa afya tuweke mipango madhubuti ya kuwalinda watoto wetu hasa katika kipindi hiki na kuwatahadharisha na kutojisaidia ovyo ovyo katika maeneo ya vichakani kwani hii ni hatari sana kupata magonjwa ya mlipuko.'' Amesema.

Aidha Kamba amesema, kwa kipindi hiki  ni lazima viongozi wa shule pamoja na mamlaka zinazohusika kuhakikisha kwamba wanazingatia maagizo ambayo yanatolewa na wataalamu wa afya ikiwemo kuzingatia usafi wa mazingira pamoja na kuweka mafi safi na salama katika maeneo ya shule ili wanafunzi wanapotoka kujisaidia waweze kusafisha na kunawa mikono yao kwa lengo la kuthibiti milipuko ya magonjwa hayo.

Pia aliongeza kuwa katika kupambana na wimbi la mlipuko wa magonjwa wanaendelea kushirikiana bega kwa bega na walimu wa shule mbali mbali zilizopo katika Mkoa wa Pwani juu ya kuwaelimisha umuhimu  wa usafi wa mazingira katika maeneo yao ya kazi na kuwapa mafunzo ambayo yataweza kuwasaidia katika kuwaelimisha watoto wao katika kujikinga na magonjwa ambayo yanatokana na uchafu.

“Suala la baadhi ya wanafunzi au jamii yoyote kuwa na tabia ya kujisaidia katika maeneo ya vichakani hii sio sahihi kabisa hata kidogo kwani ni hatari zaidi kutokea kwa magonjwa ya milipuko kama vile kuumwa na tumbo,kuhara na  kuibuka kwa  ugonwa wa kipindipindu na kitu kingine mtu anaweza kujisaidia na mvuaikaja kunyesha hivyo ikikisomba kinyesi kunaweza kuleta madhra makubwa katika jamii ambayo ipo karibu na maeneo hayo.'' Amesema.

Katika hatua nyingine Kamba aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba inaboresha sekta ya afya na kuwapatia huduma ya matibabu wananchi wake hivyo isingependa kuona hali ya kuwepo kwa magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza kuthibitiwa endapo jamii ikizingatia kanuni na taratibu zote  ambazo zinatolewa na watalaamu wa sekta ya afya ili kuondokana kabisa na hali hiyo.

                

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...