Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
SHIRIKA
la Viwango Tanzania (TBS) wamesema kwa sasa nchi ina uwezo wa kuongeza
mapato baada ya shiriko hilo kusitisha mkataba wa ukaguzi wa magari na
mawakala unaoisha mwezi Februari mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa udhibiti
wa Ubora (TBS) Lazaro Msasalaga amesema utaratibu wa ukaguzi wa magari
kuanzia mwezi Februari utafanyika hapa nchini chini ya Shirika lao.
Amesema,
TBS ilianza ukaguzi wa magari mwaka 2002 , na waliingia mkataba
na mawakala na wakawa wanafanya ukaguzi kwa niaba ya serikali na
walikua wanatoa vyeti vya ubora
Amesema,
Programu hii iliweza kusaidia katika kuleta magari yenye viwango vya
kimataifa , sasa mawakala walikua wanaingia mkataba wa miaka 3 na sasa
unamalizia hivi karibuni na magari yote yataanza kukaguliwa nchini
ambapo awali yalikuwa yanakaguliwa nje ya nchi.
Msasalaga
amesema, kuna faida kubwa sana kwa nchi kwa sababu kukaguliwa magari
hapa nchini kutapelekea nchi kuongeza mapato, kutoa ajira kwa watalaamu
na pia kujenga uwezo kwa vijana.
"Kwa
sasa tupo katika maandalizi ya kuweka sawa seti za vifaa vya ukaguzi
ambapo jumla ya seti 12 zitafungwa katika yadi zilizopo na kufanikisha
kwa suala hili litasaidia taifa katika kuongeza mapato,"
"Utaratibu
huo utasaidia pia kutoa ajira kwa vijana na ujuzi kwani tunaamini wapo
watanzania wamesomea masuala ya ufundi," amesema Msasalaga
Aidha
amesema, ukaguzi huo wa magari utafanywa ndani ya nchi kwa sasa na
itakapobainika gari haijakidhi viwango mmiliki wa gari hilo atalipia
matengenezo ya gari hilo na kisha litakaguliwa tena.
"Watu
wa forodha (clearing and forwading) watafanya utaratibu wa kawaida na
ukishakamilika wataingia kwenye ukaguzi, hilo linakuwa la mwisho baada
ya kumaliza taratibu za kiforodha,"
Aidha,
ameongezea kuwa , gharama za ukaguzi kwa gari moja ni kiasi cha
Shillingi 350,000 na serikali walikuwa wanakosa fedha hizo na kupata
asilimia 30 ya fedha za ukaguzi zilizokuwa zinalipwa wamiliki wa magari.
Mkurugenzi
wa Udhibiti Ubora Shirika la Viwango Tanzania, Bw.Lazaro Msasalaga
(katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu ukaguzi wa magari yanayotoka nje ya
ya nchi.Alipofanya mkutano na wanahabari leo Makao Makuu ya Shirika hilo
Jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...