Na Woinde Shizza, Michuzi Tv -ARUSHA

SERIKALI katika Mwaka wa fedha 2020/21imetenga Sh. bilioni 18 kujenga Chuo kipya cha Ufundi Dodoma (Dodoma Technical College)chenye uwezo wa kudahili wanachuo wapatao 1500.

Akizungumza kwenye Mahafali ya 12 ya chuo Cha ufundi cha Arusha (ATC) ambapo jumla ya wanachuo wapatao 667 walihitimu masomo ya ngazi mbalimbali na kutunukiwa vyeti,Katibu Mkuu wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Dk. Leonard Akwilapo amesema uanzishaji wa chuo hicho unalenga kuzalisha mafundi wa kutosha wenye ujuzi utakaosaidia kuimarisha uchumi wa viwanda nchini.

Aidha amesema Serikali ipo kwenye mpango wa kujenga vyuo vya ufundi Stadi 43 katika wilaya na Mikoa haoa nchini na hivyo kuongeza fursa ya upatikanaji wa elimu ya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi nchini.

Amesema katika  chuo Cha ufundi Arusha  Serikali imefanikiwa kuweka mitambo ya kisasa na vifaa vyenye thamani ya sh,bilioni 15 kwa ajili ya karakana, ujenzi wa mitambo ya magari ,Maabara ya upimaji wa udongo  pamoja na Maabara za TEHAMA ,lengo ni kuhakikisha chuo kinazalisha wataalamu wenye ujuzi utakao endana na sayansi na Teknolojia.

Awali Mkuu wa chuo hicho,Dkt Musa Chacha alisema jumla ya wahitimu wapatao 667 wamefuzu masomo yao katika ngazi ya Astashahada ya awali , Astashahada,Astashahada,Stashahada ya juu na shahada .Ametoa rai kwa wahitimu baada ya kumaliza masomo yao kwenda kutafuta fursa badala ya kusubiri fursa ziwafuate.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya utawala wa chuo Cha ufundi Arusha Profesa Siza Tumbo amesema bodi hiyo imefanikiwa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoathiri Utekelezaji wa majukumu ya chuo.Mafanikio hayo ni pamoja na suala la kuongeza bajeti ya chuo Kila Mwaka kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika kubiresha miundombinu ya chuo.

Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akiwa Katika picha ya Pamoja na mkuu wa chuo Cha ufundi Arusha pamoja na wanafunzi waliowahi kusoma Katika shule hiyo juzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...