Jane Edward, Michuzi TV,Arusha.


Shirika la ndege la Air Tanzania limerejesha  safari zake rasmi  za kuja mkoani Arusha kupitia kiwanja cha ndege cha Arusha  ikiwa na malengo ya kutangaza utalii na kusogeza huduma karibu kwa wateja.

Akizungumza wakati wa hafla ya  kupokea ndege hiyo katika kiwanja cha ndege wa Arusha,Meneja wa shirika la ndege la Air Tanzania Kanda ya kaskazini, Estermary Karumbo alisema kuwa, kwa muda mrefu walisitisha huduma kupitia kiwanja hicho  kutokana na changamoto mbalimbali ila kwa sasa wamerudi rasmi.

Alisema kuwa,uwepo wa safari hiyo utasaidia sana  kukuza utalii na kuweza kurahisisha huduma ya usafiri kwa wateja wao ,badala ya kwenda kupandia kiwanja cha Kia ambapo wanatumia muda mrefu  wataweza kutumia kiwanja hicho kwa muda mchache.

"Tunamshukuru sana Rais Magufuli pamoja na serikali yetu kwa juhudi kubwa walizofanya za kuhakikisha tunarudisha tena huduma katika kiwanja cha ndege Arusha ,ambapo ndege yetu itakuwa inatoka Arusha kupitia Zanzibar kwenda Dar es Salaam ,ambapo ni fursa Sasa kwa wafanyabiashara wetu wa mizigo kuutumia uwanja huu kusafirisha bidhaa badala ya kutumia uwanja wa Kia ili kuokoa muda ."alisema Karumbo.

Naye Meneja wa kiwanja Cha ndege Cha Arusha ,Injinia Elipid Tesha alisema kuwa,wanashukuru Sana kwa shirika hilo kurudisha huduma zake katika uwanja huo kwani inatoa fursa kubwa ya kutangaza utalii  sambamba na kuokoa muda kwa watumiaji wake.

Alisema kuwa,wameweza kufanya maboresha mbalimbali ya uwanja huo kwa kipindi Cha mwaka wa fedha 2019/2020 na 2020/2021 katika ukarabati was kiungo Cha kuingilia barabara ya kurukia ndege  kwa kiwango cha lami ,ambapo kiungo hicho kinatumika Sana hasa hasa na ndege kubwa Kama ATR 72 na Bomberdier.

Naye Rubani wa ndege kutoka shirika la Air Tanzania , Captain Michael Lengaram alisema kuwa,ni furaha kubwa Sana kwao kutua tena katika kiwanja hicho Cha Arusha baada ya kusitisha muda mrefu na hivyo historia imeweza kuandikwa tena ,hivyo wanawakaribisha sana abiria wao kuweza kukitumia tena kiwanja hicho.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...