SHULE za St Mary’s nchini zimeendelea kufanya vizuri kitaaluma katika matokeo ya darasa la nne yaliyotangazwa hivi karibuni.

Mkuu wa shule ya St Mary’s Tabata, Thomas Samson amesema licha ya kufanya vizuri mwaka jana wamejipanga kuendelea kuongoza kwenye matokeo mbalimbali kitaifa na hawatabweteka.

Amesema kwenye matokeo ya darasa la nne shule yake imefanikiwa kuwa ya 19 kati ya shule 95 wilaya ya Ilala, ya 89 kati ya shule 527 Dar es Salaam nay a 429 kitaifa kati ya shule 14, 514

Kwenye matokeo hayo, shule ya St Mary’s Mbagala ilifanikiwa kuwa ya 17 kati ya shule 107, ya 123 kati ya shule 527 mkoa wa Dar es Salaam nay a 626 kitaifa kati ya shule 14,514

Shule ya St Mary’s Mbezi imeibuka nafasi ya 24 kati ya shule 113 kiwilaya, ya 114 kimkoa kati ya shule 527 na ya 566 kitaifa kati ya shule 14, 514

Amesema matokeo hayo yamewapa faraja kwani shule zake zote za Dar es Salaam, Mbeya na Dodoma zimefanikiwa kushika nafasi za juu kwenye matokeo hayo.

 “Kwa ujumla shule zimefanya vizuri na matokeo haya ni faraja kwetu kwani tunahakikisha hatuwaangushi wazazi ambao wametuamini na kutupa watoto wao na tunaahidi kufanya vizuri zaidi kwenye matokeo yajayo,” alisema Thomas.

Aidha ametaja siri ya mafanikio hayo kuwa ni kujituma kwa walimu na nidhamu ya wanafunzi katika kufuatilia masomo na mazingira mazuri ya kusomea kwa wanafunzi wa shule hizo.

Wanafunzi wa darasa la tano ambao walifanya mtihani wa darasa la nne mwaka jana wa shule ya St Mary’s Tabata wakifurahia na mwalimu wao Daniel Seleman wakati akiwasomea matokeo ya mtihani huo ambapo wanafunzi wa shule hiyo waliofanya mtihani huo wamefanikiwa kufaulu kwa alama za juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...