Na Woinde Shizza , Michuzi Tv-ARUSHA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Arusha(TAKUKURU)
inachunguza kiasi cha sh,Milioni,933,866,399.68 zilizokopwa na SACCOS
za mashirika makubwa  ya umma  Mkoa wa Arusha AICC  SACCOS na AUWSA
SACOOS kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii PSSF na kushindwa kurejesha
kwa wakati.

Akizungumza  na waandishi wa hàbari wakati akitoa taarifa ya miezi mitatu
ya utendaji kazi ofisini kwake , Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha,
James Ruge alifafanua kwamba katika kiasi hicho SACCOS ya kituo cha
kimataifa cha mikutano AICC Saccos  ilikopa kiasi cha sh,milioni
435,754,794.46 na kushindwa kulipa kwa wakati


Aidha Saccos ya Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira Mkoa wa
Arusha AUWSA ilikopa kiasi Cha sh, milioni 498,111,609.47 na kushindwa
kurejesha kwa wakati kwa mujibu wa makubaliano na hivyo takukuru
umeanza uchunguzi was kuzirejesha kwa mujibu wa Sheria.

Aliongeza kuwa taasisi hiyo pia ipo katika hatua ya kurejesha kiasi
cha shilingi milioni 414,901,264 zilizotokana na mkopo  wa Matrekta
uliotolewa na Mfuko wa Pembejeo wa wizara ya Kilimo kwa wakulima kumi
wa halmashauri ya Meru,Arusha na Monduli Kati ya mwaka 2013 hadi 2016.

Alisema fedha hizo zilitolewa na shirika la maendeleo la Taifa NDC kwa
lengo la kuwasaidia wakulima kuondokana na umasikini wa kutumia jembe
la mkono .

Amewataka wakulima wote wa mkoa wa Arusha waliopata mkopo wa matrekta kupuuza upotoshaji unaoenezwa kwamba mkopo wa serikali kuwa
hairejeshwi.

Katika hatua nyingine Ruge amesema kwamba katika kipindi cha miezi
mitatu ya Oktoba,Novemba na Disemba TAKUKURU Mkoani humo imefanikiwa kurejesha fedha na mali zenye thamani ya sh,milioni 578,580,334..

Alisema kati ya fedha hizo sh,milioni 365,580,334 ni fedha taslimu.
Alisema fedha hizo ni Kodi ya serikali, madeni ya vyama vya ushirika
na Madi binafsi ya wananchi wanyonge yaliyokuwa kwenye hatari ya
kupotea kutokana na ubadhilifu ,dhuluma na utapeli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...