Balozi wa Norway nchini Elisabeth Jacobsen (katikati,) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la Sauti za Busara kwa mwaka huu, na kueleza kuwa jukwaa hilo ni fursa kwa watanzania na Afrika kwa ujumla katika kutangaza utamaduni wa Afrika Kimataifa, leo jijinji Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa tamasha la Sauti za Busara Yusuf Mahmoud (katikati,) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya tamasha hilo ambalo litapambwa na wanamuziki kutoka kote barani Afrika na kusema kuwa litakua kwa kiingilio cha elfu kumi kwa siku mbili na shilingi elfu sita kwa siku moja ya tamasha. Leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa umoja wa Ulaya nchini  Manfredo Fanti (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la Sauti za Busara kwa mwaka huu na kueleza kuwa hiyo ni fursa kwa watanzania na Afrika katika kuutangaza utamaduni wao kimataifa, Leo jijini Dar es Salam.

Msanii wa muziki wa Singeli Dullah Makabila (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la Sauti za Busara kwa mwaka huu, na kueleza kuwa hiyo ni fursa kubwa kwake katika kuutangaza Muziki wa Singeli kimataifa, Leo jijini Dar es Salaam.


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

TAMASHA la 18 la Sauti za Busara linatarajiwa kufanyika Februari 12 na 13 mwaka huu huko visiwani Zanzibar na kuelezwa kuwa burudani kutoka kote barani Afrika zitarindima ndani ya siku hizo mbili kwa kiingilio rafiki kabisa cha shilingi elfu sita kwa siku moja na elfu kumi kwa siku mbili za tamasha hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Tamasha hilo Yusuph Mahmoud amesema kuwa kauli mbiu ya tamasha hilo ni "Mazingira Yetu, Maisha Yetu." Imelenga kukuza ufahamu, mazungumzo na hatua za mabadiliko na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo tayari yamefikia kiwango cha dharura kote ulimwenguni.

"Shughuli zitaangazia miradi ya elimu juu ya athari za matumizi ya plastiki, uchafuzi wa bahari na ukataji miti, pia tamasha litapendekeza hatua rahisi ambazo kila mmoja wetu anaweza kuchukua ili kutimiza wajibu wa kusaidia kuokoa sayari ikiwemo kuhifadhi maji, kutumia nishati jua, kulinda mazingira ya bahari na kupanda miti.'' Amesema.

Vilevile amesema kuwa;

"Kama waandaaji, tunaamini jukumu letu kuu ni kuhakikisha tamasha linaleta matokeo chanya katika kuleta faida zinazoonekana kwa jamii ya watanzania kuwa ujumla." Amesema Mahmoud.

Aidha ameeleza kuwa tamasha hilo linalowakusanya watu wa asili tofauti katika umoja na kusherehekea ni sehemu ya kulinda utamaduni kwa  kuzingatia shughuli zinazojenga maarifa na ujuzi pamoja na kuzalisha mapato kwa wenyeji hasa wanawake, vijana na jamii zilizotengwa.

Kwa upande wa Balozi wa Norway nchini Elisabeth Jacobsen amesema kuwa kupitia tamasha hilo utamaduni wa Afrika hasa Tanzania utakua zaidi na kuweza kupata fursa ya kuonekana kimataifa.

Amesema, wasanii wengi wamekuwa wakipata fursa ya kutumbuiza kupitia tamasha hilo na kuweza kutambulika kimataifa na kuwataka watanzania na Afrika kwa ujumla kutumia fursa hiyo kwa kushiriki tamasha la Sauti za Busara mwaka huu.

Wasanii watakaotumbuiza katika tamasha hilo ni pamoja na  Barnabas Classic, Dullah Makabila (Tanzania,) Yugen Blakrok kutoka Afrika Kusini, Morena Leraba wa Lesotho pamoja na wasanii wengi kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Algeria, Ghana, Gambia, Reunion pamoja na Uganda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...