Na Said Mwishehe,Michuzi TV

TAMASHA kubwa lililopewa jina la Pamoja ambalo limeandaliwa na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania linatarajia kufanyika Januari 28 mwaka huu katika Viwanja vya Kituo cha Utamaduni cha Alliance de France jijini Dar es Salaam.

Katika tamasha hilo mbali ya kuwepo kwa mdahalo kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kimaendeleo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii na wanamuziki ambao watatumbuiza siku hiyo pamoja na kutoa elimu kwa jamii kupitia tasnia ya sanaa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha hilo, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania   Frederick Clavier amesema ubalozi huo kwa kushirikiana na baadhi ya wasanii na wanamuziki hapa nchini  wameandaa tamasha hilo ambalo kabla ya burudani kutakuwa na mdahalo.

 "Lengo la tamasha hilo ni kuimarisha ushirikiano wa nchi za Tanzania na Ufaransa katika kudumisha tamaduni zetu,"amesema na kuongeza "Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekuwa na nia ya dhati ya kuendelea kujenga upya uhusiano mzuri baina ya nchi yetu na nchi nyingine za Afrika ikiwemo nchi ya Tanzania".

Amefafanua Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania kila inapofika Alhamisi ya mwisho wa Januari kupitia Kituo chao cha Utamduni cha Alliance de France pamoja na taasisi zake huandaa tamasha hilo na mwaka huu litafanyika Januari 28.Pia tamasha hilo litahusisha wasanii wa sanaa ya uchoraji kutoka ndani na nje ya Tanzania. 

Kwa upande wake Msanii kutoka bendi ya Bahati Pili Maguzo, ametumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kufika kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo litatoa burudani na wakati huo huo kujengeana uwezo kuhusu mambo mbalimbali ya kimaendeleo.

"Tunaomba wananchi wengi kufika katika tamasha hili ambalo wenzetu wa Ubalozi wa Ufaransa wameaua kuliandaa kwa nia njema ya kuhakikisha kwanza tunaedelea kudumisha tamaduni zetu lakini pia kujengeana uwezo wa masuala mbalimbali kupitia mdahalo ambao utafanyika siku hiyo.

"Tunatarajia kuwa na watu wengi, wanafunzi kutoka Vyuo Vikuu zaidi ya 200 watashiriki, ni tamasha kubwa na la aina yake.Tunaamini katika siku hiyo kutakuwa na mambo mengi ya kujifunza pamoja na kupata burudani kutoka kwa wasanii,"amesema.

Wakati huo huo Mwanamuziki wa kujitegemea Jaffary Bandokine ameeleza amejiandaa vya kutosha kuelekea katika tamasha hilo na siku hiyo ataimba nyimbo mchanganyiko zikiwemo za Tanzania na nchi za Magharibi.Imeelezwa katika mdahalo huo Mjasiriamali na Mfanyabiashara Nancy Sumari ni mmoja ya wageni waalikwa ambao watatoa mada kwa vijana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...