WASHINDI 12 wa droo ya mwezi wa pili ya NMB Mastabata Siyo
Kikawaida, wamepatikana leo na kujizolea zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 28.8,
hivyo kufanya zawadi zilizotolewa kufikia thamani TZS 87.6 kati ya zaidi ya Sh.
Mil. 200 zinazoshindaniwa.
Promosheni ya Mastabata Siyo Kikawaida inayoendeshwa na
Benki ya NMB, ni kampeni inayolenga kuhamasisha matumizi na manunuzi kwa Kadi
za NMB Mastercard na Masterpass QR, ilianza Novemba 24, 2020, ikitoa zawadi za
Sh. 100,000 kwa washindi 40 kila wiki na washindi 12 wa Sh. Mil. 2.4 kila mwezi
kila mmoja.
Akizungumza wakati wa droo hiyo ambayo ni ya pili kati ya
tatu za mwezi, Mkuu wa Biashara ya Kadi wa NMB, Philbert Casmir, amesema katika
droo saba zilizotangulia (sita za wiki na mbili za mwezi), zimewawezesha
washindi wapatao 304 kujizolea zawadi za TZS. 87.6
Casmir amebainisha kuwa, NMB Mastabata imebakisha droo 3
kukamilisha miezi mitatu ya kampeni hiyo, ambayo zawadi kuu 'Grand Finale'
itakuwa ni ziara ya utalii Zanzibar, Ngorongoro ama Serengeti, iliyolipiwa kila
kitu na Benki ya NMB, ambako washindi watakuwa huru kuchagua zawadi mbadala.
"Wito wetu kwa wateja wa NMB kuendelea kufanya
matumizi na manunuzi mbalimbali kwa Kadi za NMB Mastercard na Mastercard QR,
ili kujiongezea nafasi sio tu ya kushinda zawadi za wiki na mwezi, bali ziara
hii ya kitalii katika moja kati ya maeneo hayo matatu." Amesema Casmir.
Katika droo ya leo, iliyofanyika chini ya usimamizi wa
Ofisa kutoka Bodi ya Michezo Kubahatisha Tanzania (GBT), Pendo Albert, washindi
12 walikuwa huru kuchagua zawadi zilizogawanywa katika makundi matatu, kila
moja likiwa na zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 2.4.
Katika kundi la kwanza kulikuwa na zawadi ya simu ya
Samsung Galaxy Note20 yenye thamani ya Sh. Mil. 2.4, kundi la pili friji, water
dispenser, Microwave na Samsung A21 kwa pamoja. Kundi la tatu ni runinga (flat
screen inchi 40) iliyolipiwa DSTV miezi mitatu, laptop na simu aina ya Samsung
A21.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...