Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.Biswalo Mganga akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera.


MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amewafutia Mashtaka washtakiwa 183 katika Magereza ya Karagwe, Bukoba, Biharamulo na Muleba mkoani Kagera.

Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP).Biswalo Mganga amebainisha alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera na kusema kuwa Mkoa huo unakabiliwa na kesi nyingi za mauaji.

Ameeleza kuwa,  baada ya kutembelea Magereza mbalimbali  na kuongea na mahabusu walioko ndani ameamua kuwafutia washtakiwa  57 toka wilaya ya  Karagwe, 54 Bukoba, 48 Biharamulo  na Muleba 26 huku katika ziara hiyo akikutana na badhi ya washtakiwa ambao ni wahamiaji haramu 15  waliokuwa wamekaribishwa na wazawa wa mkoa wa Kagera. 

"Kimsingi kuna makosa mengi na kesi nyingi ambazo walengwa hawastahili kuwemo gerezani hivyo nimeamua kuwaachia, kikubwa niwaombe viongozi wa dini muendelee kuhubiri amani,upendo ili vitamalaki kwani vitasaidia kupunguza hizi kesi." Amesema Mganga. 

Aidha, Bw.Biswalo  ametanabaisha kuwa hatosita kumchukulia hatua mtu yoyote bila kujali nafasi aliyonayo kisiasa,dini au Serikali ikigundulika kuwa amejihusisha   na vitendo vya Uhalifu ambapo amesisistiza suala la amani ni jukumu la kila mtu hivyo wanawajibika kuitunza kwa kuepuka kufanya makosa ya jinai.

Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Kagera  Ntemi Kilekamajenga amesema Mkoa wa  Kagera unaongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji ambapo amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani ili kupunguza vitendo vya uhalifu.

Jaji Ntemi amesema  kesi nyingi zinaweza kuishi kwa  njia ya usuluhishi nje ya mahakama hivyo kuipunguzia Serikali gharama za uendeshaji  wa kesi.  

Aidha, Jaji Ntemi amesema mkoa wa Kagera  kesi ambazo zipo katika hatua ya kusikilizwa zinakaribia kuvuka 450 hivyo mkoa wa Kagera  unaweza kuwa wa pili au watatu kwa Tanzania kuwa na kesi nyingi za mauaji.

Askofu wa Jimbo  Katoliki la Kayanga Almachius Rweyongeza  amebainisha kuwa  kufunguliwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  katika wilaya ya Karagwe kutasaidia wananchi kupata haki kwa wakati sambamba na kuwakumbusha viongozi wenzake wa dini kutimiza wajibu wao wa kuhubiri upendo na amani kwa mujibu wa maandiko matakatifu.

Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) mkoa wa Kagera Liberatha  Bamporiki ameeleza kufunguliwa kwa Ofisi hiyo ya Mashtaka katika wilaya ya Karagwe  kutapunguza gharama na muda mwingi waliokuwa wakiutumia kwenda Manispaa ya Bukoba kufautilia kesi zao hali itakyoaaidia kasi ya mashauri kuongezeka na kusaidia kukamilika kwa wakati.

Baadhi ya wakazi wa Karagwe akiwemo Clemence Isherenguzi na Selestine John wamesema kuwa kufunguliwa kwa ofisi hiyo ni ukombozi kwao kutokana na awali walikuwa wakitumia gharama kubwa kusafiri toka Karagwe kwenda Manispaa ya  Bukoba umbali kufauta huduma za mashtaka ambapo kwa sasa uwepo wa ofisi hiyo utasaidia kupunguza mzigo wa gharama  kwa wananchi wa wilaya ya Karagwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...