**************************************************

Na Greyson Mwase

Waziri wa Madini, Doto Biteko leo tarehe 20 Januari 2021 amekutana na uongozi mpya wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya TANZAM 2000 jijini Dodoma uliofika kwa lengo la kujitambulisha.

Kikao hicho pia kimeshirikisha Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Madini, Edwin Igenge, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba pamoja na watendaji wengine kutoka Wizara ya Madini,Tume ya Madini na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)

Wawakilishi kutoka katika kampuni ya TANZAM 2000 walikuwa ni pamoja na Mtendaji Mkuu, Stephen Mullowney, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mradi, Giancardo Volo na Andrew Cheatle.

Akizungumza katika kikao hicho Waziri Biteko ameitaka kampuni hiyo kutimiza masharti yaliyowekwa ili kuondolewa kwa hati ya makosa waliyokuwa wameandikiwa na Tume ya Madini.

Masharti hayo yalikuwa ni pamoja na kupitia na kufanya marekebisho ya mpango kazi wa uendelezaji wa mgodi huo pamoja na kuwasilisha upya, kulipa fidia wananchi wanaozunguka mgodi huo katika eneo la Katoro mkoani Geita na kupitia na kufanya marekebisho ya mkataba kati yake na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)

Awali kampuni ya TANZAM 2000 ilisaini makubaliano mwaka 2011 na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Katoro Mkoani Geita, TANZAM 2000 ikiwa na hisa asilimia 45 na STAMICO hisa asilimia 55 lakini ikashindwa kuendeleza hali iliyopelekea kuandikiwa hati ya makosa na Tume ya Madini mwaka 2019

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...