Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato(katikati), akipata maelezo jinsi Kituo cha Kupoza Umeme cha Mkoa wa Mara kinavyofanya kazi, alipotembelea kituo hicho, wakati wa ziara yake mkoani humo, Februari 26, 2021.

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato(kushoto), akionyesha katika mitambo ya kupoza umeme katika Kituo cha Kupoza Umeme cha Mkoa wa Mara, alipotembelea kituo hicho, wakati wa ziara yake mkoani humo, Februari 26, 2021.

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (kushoto), akionyeshwa kitu katika mitambo ya kupoza umeme katika Kituo cha Kupoza Umeme cha Mkoa wa Mara, alipotembelea kituo hicho, wakati wa ziara yake mkoani humo, Februari 26, 2021

 

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakati wa ziara yake mkoani Mara, Februari 26, 2021.

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, akishiriki dua na sala kabla ya kuanza kwa mkutano wake na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) alipofanya ziara mkoani Mara, Februari 26, 2021.

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (kushoto) akiteta jambo na kaimu meneja wa shirika la umeme tanzania ( TANESCO) Mhandisi Hamis Kadoma( kushoto) wakati wa mkutano wake wafanyakazi wa Shirika hilo mkoani humo alipofanya ziara Februari 26, 2021.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), mkoani Mara wakimsikiliza, Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na wafanyakazi hao alipofanya ziara mkoani humo, Februari 26, 2021.

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, akisani kitabu cha wageni alipotembelea Kituo cha Kupoza Umeme cha Mkoa wa Mara, wakati wa ziara yake mkoani humo, Februari 26, 2021.

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato(kulia), akitoa maelekezo kwa watendaji katika Kituo cha Kupoza Umeme cha Mkoa wa Mara, alipotembelea kituo hicho, wakati wa ziara yake mkoani humo, Februari 26, 2021

 

………………………………………………………………………………..

Na zuena msuya mara

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, ametaka wafanyakazi wa shirika la umeme tanzania ( TANESCO) kufanya kazi kwa kasi, ubunifu na usahihi kwa maslahi mapana ya nchi na taifa kwa jumla.

Wakili Byabato alisema hayo wakati wa ziara yake mkoani Mara, Februari 26,2021,  ambapo alizungumza na wafanyakazi wa (TANESCO) pamoja na kutembelea Kituo cha Kupoza Umeme cha  mkoa huo kinachozalisha Megawati 24, matumizi halisi kwa sasa yakiwa ni megawati kumi nukta saba (10.7).

Alisema kuwa kwa kufanya kazi kwa kasi, ubunifu na usahihi kutawezesha shirika hilo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuwahudumia watanzania wote kwa wakati sahihi.

“Wafanyakazi wa TANESCO wanadhamana kubwa ya kuhakikisha kuwa umeme unasambaa Tanzania nzima kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, ni wakati sahihi kufanya kazi kwa kasi, ubunifu na usahihi ili kutimiza azma ya serikali ya kufikisha umeme kwa watanzania wote na kukuza uchumi wa viwanda”, alisema  Wakili Byabato.

Akizungumzia kituo cha kupoza umeme cha mkoa wa Mara, alisema kuwa kituo hicho kilizinduliwa mwaka 1989 na kinapokea umeme kutoka katika maeneo manne (Fider) ambayo ni katikati ya mji wenye wa Mara, Butiama, Tarime na Majita.

Aidha alisema kuwa, hivi karibuni serikali inatarajia kutanua   kituo hicho ili kongeza uwezo wake wa kuzalisha umeme.

Vilevile aliwataka wawekezaji kuwekeza katika mkoa huo kwa kuwa kuna umeme mwingi na wa kutosha. 

Katika hatua nyingine aliwataka watanzania kulinda miundombinu ya umeme iliyopita na kusambazwa katika maeno yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...