Mkuu wa wilaya ya Arusha Kennan Kihongosi akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mazoezi ya  IAA.

Mkuu wa wilaya ya Arusha ,mkuu wa chuo Cha
uhasibu pamoja na washiriki wengine wakiendelea na mazoezi ya viungo
Katika viwanja vya chuo hicho.
Mkuu wa chuo Cha uhasibu Profesa Eliamani
Sedoyeka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mazoezi ya  mbio  fupi maarufu
kama IAA fun run.

Na Woinde Shizza , Michuzi Tv -ARUSHA

CHUO cha uhasibu Arusha kimeanzisha mazoezi ya mbio fupi maarufu kama
IAA fun run  yatakayofanyika kila mwezi ikiwa ni maandalizi kuelekea
mbio ndefu za marathon zinazotarajiwa kufanyika  Mei 2021.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mbio hizo mkuu wa chuo hicho Profesa
Eliamani Sedoyeka alisema kuwa wameanza kukimbia kilometa saba na nusu
ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wanafikia malengo yao ya muda mrefu ya
kuwa na marathon.

Alisema kuwa IAA marathon lengo lake kubwa ni kukitangaza chuo kwani
ndio msingi mkubwa wa biashara ambapo wanapokuwa wamekikuza chuo
watakuwa na mvuto zaidi kwa wateja na hiyo ni moja kati ya mikakati
yao kwa kuja na shughuli za kitaifa ambazo zitaweza kuvutia watu.

Alieleza kwa chuo hicho ni sehemu ya Arusha hivyo lengo lingine ni
kukuza utalii wa ndani na nje  ambapo kwa kufanya marathon hiyo
wanatarajia kufuta watu kutoka maeneo mbali mbali ya ndani ya nchi na
mengine.

Alisema Lenggi lingine kuinyanyua na kukuza vipaji vya kukimbia kwani
Tanzania hivi karibuni imekuwa kama kivutio cha watu kufahamiana, kuwa
na undugu lakini pia kushereheka zaidi ambapo wamatamani siku moja
timu ya riadha ya taifa ije kuwa na makao yake katika chuo hicho.

"Arusha iko nyanja za juu maana yake ni maeneo mazuri kabisa ya
kufanya mazoezi ya mbio ndefu kwahiyo tunategemea kwamba IAA marathon
italeta upizani mkubwa sana katika marnyingi na sisi tumejipanga
kuhakikisha kuwa wale wote tutakao waalika watawashindanisha na kutoa
mabingwa ambao wataweka rekodi za kitaifa kwenye kilometa 21 na 47,"
Alisema Professa  Sedoyeka.

Alifafanua kuwa hivi karibuni walisaini mkataba na chama cha mpira
Tanzania(TFF) kwajili ya kunyanyua mpira wa miguu ambapo
walishaanzisha ufadhili wa mpira wa huo na kwasasa ni kwaajili ya
kukimbia.

Aidha kuhisiana na mazoezi Profesa Sedoyeka alisema kuwa  ni muhimu
kukumbuka  ili mtu aweze kuwa na akili nzuri awe ni mwanafunzi au
mwalimu uwezekufundishwa au kujifudha mwili unanafasi kubwa sana kwani
kwa kufanya mazoezi mtu anaweza kuondoa mawazo(stress).

"Pamoja na kuondoa stress lakini pia unajenga mwili kwa kuweka vizuri
usawa wa sukari, chumvi na madini mengine yaliypo mwilini pamoja na
kuchochea unywaji wa maji  ambo unapelekea kuweka misuli, na damu sawa
pamoja na kwenda kuondoa yale magonjwa yasiyoambukizika kama sukari,
moyo, msogo wa mawazo na mengine," Alisema

Alisema kuwa kuwa sasa hivi sera ya taifa ya afya inalenga kwenye
magonjwa ambayo yalikuwa yamesahaulika ambapo kwa watu wa tasnia yao
ambao wanakaa sana na kutumia akili nyingi ndo wako hatarini hivyo kwa
kuanzisha shughuli hizo za mazoezi watalinda rasilimali watu vizuri na
kupelekea kuongeza ubunifu kwa manufaa ya chuo na taifa kwa ujumla.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi alisema kuwa
mazoezi ya poamoja waliofanya kwa kushirikiana na chuo cha uhasibu
yatajenga ushirikiano mzuri kati ya wanafunzi, viongozi na wananchi
ambapo anaamini kiwa katika ushirikiano na kufanya kazi pamoja lakini
pia mazoezi ni afya.

"Sisi kama serikali tunayapongeza mazoezi haya na tumeyabariki na
tutazidi kuja kila watakapoandaa kwani yanaleta mahusiano mazuri na
nikichocheo kizuri cha uchumi,"Alisema Kenan.

Alisema kuwa wanapofahamiana wanaweza kufanya shunguli mbalimbali za
aidha za kizalendo kama vile ujenzi wa madarasa biashara na mengine
mengi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...