Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Dk.Tito Mwinuka akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya Wahariri na maofisa waandamizi wa Shirika hilo.Ufunguzi wa rasmi kikao hicho umefanywa na Waziri wa Nishat Medard Kalemani leo Februari 27,2021 Mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abass akizungumza wakati wa kikao kazi hicho ambapo amesisitiza umuhimu wa taasisi za umma kuhakikisha zinatoa taarifa kwa umma na kwa vyombo vya habari nchini.
Mijadala ikiendelea.
Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani (katikati) akiwa na maofisa wa TANESCO pamoja na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari katika picha ya pamoja baada ya kufunguliwa kwa kikao kazi leo Februari 27,2021 Mjini Morogoro.

Mjadala ukiendelea.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Morogoro

MTENDAJI Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Dk.Tito Mwinuka amesema kwamba Shirika hilo linajukumu kubwa la kuleta mabadiliko kwa jamii za Watanzania mijini na vijijini kwa kuwapatia nishati ya umeme ya uhakika na kwa bei nafuu.

Dk.Mwinuka hayo amesema hayo leo Februari 27,2021 kwenye kikao kazi kati ya maofisa wa shirika hilo na wahariri wa vyombo vya habari ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani.

Amefafanua katika kufanikisha hilo, Shirika limekuwa  likitekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati itakayosaidia kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na ustawi endelevu wa uchumi  wa nchi yetu. 

Ameweka wazi katika uzalishaji Umeme, Serikali kupitia TANESCO inatekeleza mradi mkubwa wa kufua umeme wa maji wenye uwezo wa Megawati 2115 wa Julius Nyerere utakao gharimu Sh.Trilioni 6.5 fedha za watanzania. Pia wanayo miradi kama vile Rusumo (MW 87) ambapo hadi sasa utekezwaji wake umefikia asilimia 76.8 na utagarimu Sh. billioni 263.

"Hata hivyo Serikali kupitia TANESCO, inatarajia kutekeleza miradi mingine mikubwa kama vile Ruhuji 358 MW, Rumakali 222MW, Mtwara MW 300, Somanga fungu MW 300, Kakono MW 87, Malagarasi 45 MW,"amesema.

Dk.Mwinuka amesema kupitia utekelezaji huo wa miradi hiyo ya uzalishaji umeme, wanategemea hadi kufikia mwaka 2025 TANESCO kuwa na uwezo wakuzalisha Megawati 5,000 na hiyo itasidia nchi kuwa na umeme wa kujitosheleza na utakaochochea ukuwaji wa uchumi na kuuza ziada itakayobakia nje ya nchi.  

Aidha amesema Shirika linatekeleza miradi mbalimbali ya kusafirisha umeme nchini kama vile, 400Kv Kenya -Tanzania Interconnector, 400Kv Tanzania – Zambia Interconnector, 400Kv Julius Nyerere hadi Chalinze na 400kV Kigoma – Nyakanazi. 

"Miradi hiyo yote itasaidia kusafirisha na kuimarisha hali ya umeme katika gridi ya Taifa  nchini pamoja na kuwezesha biashara ya kuuziana umeme baina ya nchi majirani. Shirika pia ina tekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji umeme katika Mikoa, vijijini na Mijini.

" Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme utakaotumika katika treni ya SGR Awamu ya Kwanza (Lot I) nao umekamilika kwa asilimia 100,"amesema Dk.Mwinuka wakati anazungumza kwenye kikao hicho.

Wakati huo huo amesema kwa sasa uwezo wa TANESCO kuzalisha umeme megawati  1,602.04 wakati mahitaji halisi ya wateja ni megawati  1,180.53."Mtaona tuna ziada ya takribani megawati 520.51. 

"Hii inamanisha umeme upo wakutosha wananchi na wawekezaji wanatakiwa kuchangamkia fursa hii ya umeme kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.Takribani asilimia 87 ya watazania wameweza kufikwa na huduma ya umeme hivi sasa,"amesema Dk.Mwinuka.

Ameongeza kwamba TANESCO pia ina kampuni tanzu matatu ambayo ETDCO inashughulika na ujenzi na ukarabati wa njia za usafirishaji umeme, TGDC yenye jukumu la kuendeleza nishati ya Jotoardhi na TCPMC wao wanashughulika na utengezaji wa nguzo za zege, na wote watatoa elimu juu ya shughuli zao katika semina hii ya siku mbili hapa Morogoro.

Amesema TANESCO imejikita katika kuimarisha sekta hiyo muhimu ya umeme kwa kutafiti, kuanzisha na kuendeleza miradi mbalimbali hivyo, kupitia kikao kazi hicho cha Wahariri wataweza kupata elimu ya kutosha kuhusu shirika hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...