MWENYEKITI wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo, amewaongoza wajumbe wa mfuko huo kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambayo inatarajiwa kupatiwa fedha na mfuko huo.

Katika ziara hiyo Profesa Kitila aliambatana na wajumbe wa Mfuko huo wa Jimbo ambao ni Diwani wa Kata ya Makurumla, Bakari Kimwanga, Diwani wa Viti Maalumu, Hawa Abdulrahman.

Wengine ni Isihaka Waziri, Rozina Kimario pamoja na mchumi, ambapo hatua hiyo imetokana na uamuzi wa kamati hiyo kutembelea miradi yote kwenye jimbo kabla ya kuanza kutoa fedha.

Kutokana na changamoto kadhaa zilizopo katika kata nane za Jimbo la Ubungo ambazo ni Ubungo, Kimara, Makuburi, Sinza, Mburahati, Makurumla, Mabibo na Manzese wajumbe kwa kauli moja waliamua kwenda kufanya ukaguzi wa miradi hiyo ili kujiridhisha kama ina vigezo vya kusaidiwa kwa haraka.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila aliwaambia wananchi wa kata za Makurumla, Manzese na Mabibo kuwa Serikali imetoa kiasi cha Sh milioni 70.6 kwa ajili ya kuchochea maendeleo kwenye jimbo hilo.

Amesema wajumbe kwa kauli moja wamekubaliana kutoa kipaumbele cha fedha katika miradi ya elimu, afya na miundombinu hasa ya babarabara na vivuko ambavyo vimekuwa kero kubwa kwa wananchi.

“Tumetembea hapa Mto China na tumeona hali ya takataka zinazosafirishwa na maji namna zilizoziba mto nasi kupitia Mfuko wa Jimbo tutaingiza kiasi cha fedha ili kisaidie kazi hii ambayo chini ya diwani ataisimamia.

Pia tutasaidia barabara muhimu ya kwa Mloka Mtaa wa Kilimahewa ila kubwa tunawaomba watalaamu wa Tarura watusaidie gharama ili tuweze kukamilisha kazi hii kwa wakati.

“Tunataka fedha hizi zinazotolewa na Serikali ziende zikaguse maendeleo ya wananchi moja kwa moja,nasi kupitia Kamati ya Mfuko wa Jimbo kila senti ambayo tutapokea kutoka serikalini tutaweka wazi na wala si kificho,” amesema Profesa Kitila

Pamoja na hali hiyo wajumbe hao walitembelea Kata ya Mabibo na kuona athari za Mto Gide pamoja na Mto Mbokomu Kata ya Manzese.MWENYEKITI wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo akiwa ameongoza na wajumbe wa Mfuko huo wa Jimbo ambao ni Diwani wa Kata ya Makurumla, Bakari Kimwanga (kulia), Diwani wa Viti Maalumu, Hawa Abdulrahman (hayupo pichani) wakikagua miradi ya jimbo
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...