****************************************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MAHAKAMA ya Wilaya ya
Bagamoyo ,mkoani Pwani imewahukumu wahamiaji haramu 83 kwenda jela
miaka miwili kwa tuhuma za kuingia nchini bila vibali ikiwa ni kinyume
cha sheria.
Aidha , raia wa Tanzania wawili wamehukumiwa miaka 20 jela kwa tuhuma za kukutwa wakiwa wamewahifadhi wahamiaji haramu hao.
Katika hukumu
iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo Mwanakombo
Mmanya,ilisema raia wa Ethiopia 81,Somalia mmoja na Malawi mmoja
wamehukumiwa kwenda jela miaka miwili au kulipa faini Shilingi 500,000
kila mmoja.
Awali mwendesha
mashitaka wa Idara ya Uhamiaji ,Mkoa wa Pwani Fadhili Festo alisema
kuwa wahamiaji haramu hao walikamatwa mwezi Januari na Februari mwaka
huu katika maeneo tofauti ya Wilaya ya Bagamoyo.
Hata hivyo ,Hakimu
Mkazi wa Mahakama hiyo Mwanakombo Mmanya alimhukumu Julius Shija mkazi
wa Makurunge Bagamoyo miaka 20 jela au kulipa faini ya Shilingi Milion
20 ikiwa ni baada ya kesi yake ya kukutwa na hatia ya kuwahifadhi
wahamiaji haramu 16 nyumbani kwake.
Mwingine
aliyehukumiwa ni Eliah Lekule mkazi wa Arusha ambaye alihukumiwa miaka
mitatu jela baada ya kukutwa na hatia akiwasindikiza wahamiaji haramu
wawili katika stendi ya mabasi ya Bagamoyo kuelekea Mkoa wa Dar es
Salam.
Kufutia hukumu hiyo,
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Pwani Paul Eranga aliwaonya wamiliki
wa mabasi wanaotumika kuwasafirisha wahamiaji haramu.
“Kwasasa wahamiaji
haramu wanaopita katika Mkoa huu wamebadilisha njia ambazo walikua
wakitumia awali za kupanda boti na bodaboda badala yake sasa
wanasafirisha kwa mabasi ya abiria” anasema.
Alieleza ,basi lolote
litakalokamatwa likiwa limebeba wahamiaji haramu baada ya kesi
kumalizika litataifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Eranga pia aliwaonya
raia wa Tanzania ambao wamekuwa na tabia ya kuwahifadhi na kuwasaidia
wahamiaji haramu kuvuka hapa nchini kuacha mara moja biashara hiyo kwani
kwa atakayekutwa na hatia hatua za kisheria zitachukiwa kama onyo kwa
wengine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...