NA ANDREW CHALE, CHALINZE

WAZIRI wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Joackim Mhagama amefanya ziara na kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa Halmashauri ya Chalinze kwa fedha zilizotolewa na Benki ya dunia na kusimaniwa na TACAIDS na TANROAD ili kusaidia mapambano dhidi ya UKIMWI  kwa watu wanaoishi eneo la mradi na wale wanaopita katika eneo hilo kama wasafiri na madereva wanaopumzika katika maeneo ya Chalinze kabla yakuendelea na safari zao ndani na nje ya Nchi ikiwemo nchi za Maziwa Makuu.

Mhe. Jenista Mhagama alibaini ucheleweshwaji wa ukamilishaji wa Miradi hiyo inaotekelezwa Katika Kituo cha Afya Chalinze na Mdaula licha ya fedha za utekelezaji kuwa zimekwisha lipwa tangu mwezi Januari mwaka huu.

Akitoa kauli juu ya kusuasua kwa ujenzi huo kwa Mkandarasi, Waziri alisema:

"Sijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huu ukizingatia fedha kwa ajili ya ukamilisha wa kazi mliopewa imekwisha lipwa tangu Januari mwaka huu". Alisema Mh. Mhagama

Aidha, alimtaka Mkandarasi aliechukua mkataba wa kutekeleza ujenzi wa zahanati ya Mdahula, Maabara na Jengo la ushauri nasaha kwa watu wenye maambukizi Kituo cha afya Chalinze na Mdaula kuhakikisha anakamilisha ndani ya miezi miwili na yeye mwenyewe atakuja kulifungua mwisho wa mwezi wa nne.

'Ninawaagiza miradi yote mliopewa kutekeleza hakikisheni inakamilika kabla ya tarehe 25.04.2021 na  nitatuma maafisa toka ofisi yangu kuja kukagua na tarehe 30.04.2021 nitakuja kuzidua huduma katika majengo haya pale nitakapo jiridhisha kuwa yamekamilika kwa viwango vinavyohitajika'  Alisema Mh. Mhagama

Aliongeza kwa kusema, kuwa:
"Lengo la Serikali yetu ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wetu Msikivu Mh. Dr John Pombe  Magufuli ni kuhakikisha huduma zinazohusu mapambano dhidi ya ukimwi zinapatikana kila eneo kwa lengo la Kutoa elimu ya mapambano dhidi ya UKIMWI,Upimaji na Utoaji dawa za kufubaza virusi vya ukimwi zinapatikana kila sehemu, Aliongeza Waziri Muhagama.

Aidha, alisema uwepo wa janga la ugonjwa huo wa Virusi vya Ukiwmi ikiwemo nchi za  Afrika Magharibi na Pembezoni mwa Janga la Sahara ikiwemo Tanzania,  Jambo hilo lilipelekea Serikali kutenga bajeti na kwa kutumia wahisani kujenga vituo hivi 20 nchi nzima ili kuzidisha mapambano haya dhidi ya UKIMWI.

Ambapo zaidi ya Fedha za kitanzania Milioni 600 zimeletwa  Chalinze ili kukamilisha ujenzi wa Jengo la ushauri na nasaha na Maabara kituo cha Afya Chalinze na Zahanati ya Mdaula.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete katika ziara hiyo alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuendelea kuijali Chalinze kwani nje na Milioni 600 ambazo ametoa kwa ajili ya miradi aliokuja kuikagua Mhe. Jenista Mhagama takribani Fedha za kitanzania Bilioni Moja zimeletwa kwa ajili ya Ujenzi wa jengo la huduma ya mama na mtoto Hospitari ya Wilaya Chalinze iliopo Kata ya Msoga.

Ambapo alisema jengo hilo litasaidia kunusuru maisha ya wajawazito akina mama waliojifungua na watoto.

Mbunge alimpongeza Mhe. Jenista Mhagama kwa kuteuliwa kuwa waziri na kutaka aendeleze kasi aliokuanayo katika kusimamia Wizara hiyo ili mambo yote ambayo yamekua yakikwama yaweze kufanikiwa kwa mustakabari wa Wanachalinze na Taifa kwa ujumla.

"Nina laani vikari juu ya ucheleweshwaji wa miradi hii ulioitembelea leo kwa kua hapakuwa na sababu kwani Kampuni lililopewa mkataba wa ujenzi (Kihure Company Ltd) mlishalipwa fedha za mradi.

Nakushukuru kwa maagizo yako kuwa ndani ya miezi miwili miradi yote miwili iwe imekamilika nami kama kiongozi wa eneo hili nakuahidi kufuatilia kwa karibu maendeleo ya ujenzi huo kwa kushirikiana na viongozi wenzangu akiwemo Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri Jeofrey Kamugisha Diwani wa Bwilingu Mhe. Nasarr Karama na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Ndugu. Ramadhani Possi". Aliongeza Mhe. Ridhiwani Kikwete.

Miradi hiyo tayari baadhi ya maeneo imeshakamilika na kufanya kazi ambapo kwa Halmashauri ya Chalinze, inatarajiwa kuokoa maisha ya watu wengi kwa siku inakadiliwa kulaza malori zaidi ya 1000.








 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...