Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akisisita za jambo juu ya imeandaa Tamasha la 114 la Kumbukizi la Vita vya MajiMaji na Tamasha la Utalii wa Utamaduni mjini Songea.

******************************

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Tamasha la Kumbukizi ya Vita Vya MajiMaji na Tamasha la Utalii  wa Utamaduni litakalofanyika mjini Songea tarehe 27 Februari 2021. Tamasha hili litazinduliwa rasmi tarehe 25 Februari na Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga Jijini Dar es Salaam huku akileza malengo ya maadhimisho hayo kuwa nia pamoja na ni kuwakumbuka mashujaa wetu waliopigana vita vya MajiMaji na kufa wakitetea maslahi mapana ya nchi yetu, ikiwamo mashujaa wapatao 67 walionyongwa na Wakoloni Mjini Songea mnamo tarehe 27/02/1906 na kuzikwa katika makaburi yaliyopo Makumbusho ya MajiMaji.

Pili, ni kutoa fursa kwa Wananchi wa Tanzania kuenzi, kutunza, na kuendeleza urithi wa utamaduni na wa asili kwa ajili ya kizazi cha sasa na vijavyo. Tatu, ni kuthamini mchango wa wazee na viongozi waliotangulia akiwemo Marehemu Dkt. Lawrence Mtazama Gama katika kuleta maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma na ukanda wa Nyanda za Juu Kusini kwa ujumla ili kuinua uchumi na kuboresha hali ya maisha ya wananchi wa eneo hili Hivyo, napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wananchi wote katika tamasha hili ambalo linafundisha na kutukumbusha historia muhimu ya nchi yetu” Aliongeza Dkt Lwoga.

Nae Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi Bw Chance Ezekiel amesema kuwa licha ya kuwepo na program za Kongamano, Utamaduni wa Wangoni, Gwaride la heshma pia kutakuwa Tarehe 22-24 Februari 2021, kutakuwa na programu mbalimbali za Kielimu mashuleni, na maeneo mbalimbali ya wazi pamoja na maonesho ya wajasiliamali  na taasisi mbalimbali za binafsi na serikali. Lengo ni kuelimisha jamii historia ya nchi yetu na kuhamasisha jamii kutumia na kurithisha urithi wetu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho

“Tarehe 26 Februari 2021 ni siku ya kutembelea vivutio vya utalii wa asili na utamaduni Mjini Songea, ikiwamo eneo la Maposeni, Peramiho, mahali ambapo maji ya Vita vya MajiMaji yalianza kugawiwa na mwanamke Nduna Mkomanile. Aidha, Maposeni ni makazi ya Chifu Emmanuel Zulu ambaye ni Chifu wa kabila la Wangoni. Chifu Zulu amewaalika Machifu wengine kutoka Malawi, Zambia na Tanzania. Huko Maposeni kutakuwa na sherehe za Wangoni (Siku ya Wangoni), ikiwa ni pamoja na vyakula vya asili, ngoma na nyimbo za utamaduni” Alisema Bw Ezekiel

Maadhimisho haya ni moja ya mkakati wa Serikali wa kutangaza na kukuza utalii wa malikale na utamaduni kwa kutumia matamasha na ili kuenzi wazee waliopigana katika vita hivyo vya MajiMaji, kauli Mbiu ya mwaka huu 2021 ni: “Maisha ya Wazee Wetu, Fahari Yetu (The Legacy of  Our Elders,  Our Pride).”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...