Na Woinde Shizza , Michuzi Tv -Arusha
Akiongea na
vyombo vya habari ofisini kwake mwenyekiti wa TAMIDA Taifa,Sammy Mollel
ameeleza kwamba TAMIDA imeshitushwa na kifo cha hayati Magufuli kwani
alikuwa mwamba aliyefanikiwa kuzalisha mabilionea kupitia sekta ya
Madini.
Alisema kuwa
Magufuli alifanikiwa kudhibiti utoroshwaji wa madini kwa kujenga ukuta
Mererani,Kuanzisha masoko ya madini Nchi nzima na hivyo kupelekea
kuongezeka kwa pato la taifa kupitia sekta hiyo.
"Sisi
wafanyabiashara wa Madini TAMIDA tunatoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa
kuondokewa na hayati John Magufuli kwani tunakumbuka mageuzi makubwa
yaliyofanywa na serikali yake katika sekta ya Madini"alisema
Mollel
ameeleza kuwa TAMIDA inakumbuka jinsi hayati Magufuli alivyochangia
kulipaisha Taifa kiuchumi hadi kufikia uchumi wa Kati huku sehemu ya
pato hilo la taifa likiongezeka kupitia sekta ya madini.
Aidha
ameongeza kuwa Magufuli alikuwa na uwezo wa kubuni na kutekeleza miradi
mbalimbali mikubwa ya kimkakati nchini ikiwemo kuboresha miundo mbinu
kwa mtandao wa Lami,ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge).
Miradi
mingine ni pamoja na kufufua shirika la ndege ATCL kwa kununua ndege 7
zikiwemo mbili kubwa Aina ya Boeing 787 ,Dreamliner na kufanikiwa
kusomesha bure wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari .
Alisema
pamoja na mafanikio hayo Hayati Magufuli alilenga kuwasaidia wanyonge
wanaodhulumiwa haki zao na kusaidia wafanyabiashara wadogo wadogo
kutonyanyaswa mijini.
Mwenyekiti wa TAMIDA Sammy Mollel akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...