Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dkt Godwin Mollel akizunguza na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kwenye ziara yake iliyolenga kuangalia shughuli za utoaji wa huduma za afya na kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini, Abdulaziz Abood. (Picha na John Nditi).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dk Godwin Mollel ( kati kati suti mbuu) akiwasalimu na kuwasililiza wagonjwa waliolazwa wodini katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro na ( mbele yake ) ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini, Abdulaziz Abood, (kulia) ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo , Dk Rita Lyamuya.

Na John Nditi, Morogoro
NAIBU Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dk Godwin Mollel ameliomba Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya dola kufanya kazi zao kwa uweledi katika kushughulika na wezi wote wanakamatwa wanauza dawa za binadamu katika maduka binafsi zenye nembo ya Serikali (MSD) kwa lengo la kukomesha ufidasi wa dawa za umma.

Naibu Waziri alisema hayo wakati akizungumza na watendaji wa sekta ya afya na viongozi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro alipokuwa eneo la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kuona shughuli za uendeshaji wa huduma za afya na kupata ufafanuzi kuhusu wizi dawa za Serikali zizokamatwa katika duka moja na kudaiwa zimetoka kwenye Kituo cha Afya cha Mazimbu ambacho kinamilikiwa na Chuo Kikuu hicho.

Dk Mollel ,alisema Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imefanya kazi nzuri ya ukaguzi katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya na kwa Morogoro iliweza kukamata dawa za binadamu mitaani ambazo zimetoka Bohari kuu ya Dawa.

Naibu Waziri alisema , lakini dawa hizo zikakutwa kwenye duka binafsi ambazo zinaonekana hazijanunuliwa kwa utaratibu ambao unaotakiwa na zimeingia kwa namna ambazo zikitokea kwenye hospitali kwa madai ya awali ya mtuhumiwa aliyekamatwa akidai zimetoka Kituo cha Afya cha nje ya Chuo kinaitwa cha Mazimbu.

“ Sasa na mimi nikasema ok sisi kazi yetu ni kutafuta hao mashino ya dawa zinapotelea , nikasema niende moja kwa moja hadi kwenye tukio , kujifunza kwa macho yangu na kusikiliza namna nzuri ya kujua kwa sababu tunataka tunapokaa wizarani tujue kikamilifu kinachotokea ili tuzube miaya hiyo “ alisema Dk Mollel.

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Kanda ya Kati , Sonia Mkumbwa , kuwa Februari 18, mwaka huu (2021) katika ukaguzi uliofanyika mkoani Morogoro kwenye vituo mbalimbali vya dawa za binadamu zikikamatwa dawa yenye thamani ya Sh :1,219,150 katika duka la mtu binafsi ambazo zimetoka Bohari kuu ya Dawa (MSD).

Hivyo Naibu Waziri Dk Mollel ,alisema katika suala la wizi wa dawa za serikali na kuuza dawa bandia katika maduka ya dawa , kuwa watu wanaokamtwa vyombo vya vyote vya dola vinavyohusika vikahikishe lazima watu hao wawajibika kwa nguvu zote .

“ Kwenye hili suala la kuuza dawa feki kule Mbeya nasikia watuhumiwa wanahangaika kwa njia mbalimbali , sisi tunaviambia vyombo vyoye vinavyohusika vihakikishe waliokamatwa lazima wawajibike kwa nguvu zote “ alisisitiza Dk Mollel

Pia Naibu Waziri alitumia fursa hiyo kuwaomba watumishi wa Afya kuwa , wizara yao inawapenda , inawaheshimu na kutambua mchango wao mkubwa ambapo asilimia zaidi ya 99 wanafanya kazi vizuri na kwa uadilifu, isipo kuwa wachache wenye kutia doa na kuharibu sifa za watumishi wengine , Serikali chini ya wizara hiyo itashughulika nao kwa kutioa maamuzi magumu.

Mbali na hayo pia alikishukuru Chuo Kikuu cha SUA kushirikiana na wataalamu wake Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwenye masuala ya utafiti ambao unaleta matokeo mazuri kwa afya ya binadamu mbali na uhirikiano kwenye nyanja ya afya.

Naye Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini, Abdulaziz Abood alimshukuru Naibu Waziri huyo kutembelea Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro ili kujua changamoto zinazoikabili ili kuwezesha kuboresha huduma za afya pamoja na maslahi ya watumishi wa sekta hiyo na mkoa kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...