NAIBU  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Pauline Gekul ,ameagiza baadhi ya viongozi waliohusika kuuza eneo la shamba la Taasisi ya Chanjo (TVI) Kibaha na  wananchi wasiendelee kuuziana sehemu hiyo hadi pale wizara ya ardhi itakapotoa tamko juu ya watu waliovamia shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 1,037  .

 

Gekul alitoa rai hiyo, mjini Kibaha alipotembelea kituo hicho ambapo zamani lilikuwa shamba la kuzalishia ngombe wa kisasa (Mitamba) kuwa viongozi hao wameendelea kuwauzia watu eneo hilo mali ya serikali chini ya wizara ya mifugo na uvuvi.

 

Alisema ,baadhi ya viongozi hao wamewauzia wananchi huku wakijua kuwa wanafanya kinyume cha utaratibu.


 Aidha alisema kuwa wao kama wizara wanalifanyia kazi kujua kama wahusika walipata kihalali watawaachia na wale waotakiwa kuondoka waondoke ili mambo yaendelee.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhandisi Martin Ntemo alisema kuwa walitoa maelekezo kwa wavamizi hao kuondoka na kwa wale waliojenga wabomoe wenyewe kabla serikali haijachukua hatua ya kubomoa na wasiendeleze chochote .

 

Ntemo alisema kuwa walitoa tamko la kuwataka wananchi hao wabomoe wenye kabla ya kuja kuondolea na walitakia kuondoka hadi ifikapo Februari 19 mwaka huu .

 

Naye Meneja wa kituo cha chanjo Kibaha Dk Stella Bitanyi alisema kuwa shamba hilo lilikuwa kubwa likamegwa Halmashauri wakakabidhiwa baada ya tathmini wakaambia waendeleze hekta 2,963 na wao wakabakiwa na hekta1,037 lakini bado wananchi waliendelea kulivamia.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...