Na Said Mwishehe,Michuzi TV.

MSANII maarufu nchini Tanzania na Bara la Afrika Nasseb Abdull 'Diamond Platnumz' amesema amefurahishwa na vivutio vya utali ambavyo vipo katika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani huku akieleza atakuwa balozi wa kuitangaza Wilaya hiyo kwenye eneo la utalii na fursa za uwekezaji.
Aidha ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa hatua mbalimbali ambazo inachukua katika kuboresha maeneo ya hifadhi za utalii na vivutio vyake na kuvifanya kuwa vya kisasa na akiwa Kisarawe ameshuhudia ubunifu uliotumika kuboresha maeneo ya vivutio vya utalii.

Akizungumza akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jocate Mwegelo ikiwa ni matayarisho kuelekea Kisarawe Ushoroba Festival ambalo ni maalum kuutangaza utalii wa wilaya hiyo pamoja na vivutio vyake kuanzia Machi 5 hadi Machi 7 mwaka huu,Diamond amesema kuna kila sababu ya Watanzania kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya hiyo.

 "Ni jukumu letu sisi vijana tukiwemo wasanii kutumia kutangaza utalii na fursa zilizopo,huko nyuma wasanii walikuwa wakienda nchini Afrika Kusini ili kurekodi video zao lakini tunashukuru Serikali ya Awamu ya Tano imerahisha na kuweka mazingira mazuri ya kurekodi.

"Hivyo wasanii tunaweza kurekodi nyimbo zetu hapa hapa nchini kwenye maeneo yetu ya utalii ambayo yamewekwa kisasa zaidi.Nitoe ombi kwa watanzania kutembelea vivutio vua utalii,"amesema.
Kuhusu fursa za uwekezaji katika Wilaya ya Kisarawe, Diamond amesema ametembelea maeneo ya utalii pamoja na maeneo mengine ameshuhudia mazingira mazuri ya uwekezaji."Nimekuja Kisarawe nikiwa na watalaamu wa masoko na biashara, hivyo tutaangalia namna ya kufanya ili tutakapoamua kuwekeza basi wengi wanufaike na Serikali ipate kodi kupitia uwekezaji wetu.

"Maana uwekezaji mzuri ni ule unaonufaisha watu wengi na sio mtu mmoja peke yake.Hivyo kuelekea Ushoroba wa Kisarawe Festival , ni jukumu letu watu wengi kuja katika siku hizo kwani itakuwa fursa ya kukutana na kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.Alipoulizwa kitu gani ambacho kimemvutia ndani ya Wilaya ya Kisarawe kwenye eneo la utalii,Diamond amesema amevutiwa na mazingira mazuri na ya kuvutia yaliyopo lakini kubwa zaidi ni panzi mwenye rangi za bendera ya Taifa.

"Kitu ambacho kimenivutia ni mazingira ambayo nimekutana nayo, nimevutiwa na panzi mwenye bendera ya taifa na kubwa zaidi ni namna ambavyo Kisarawe imeamua kumtumia panzi huyo kama nembo ya Kisarawe, yule panzi nimemuaona nimemshangaa."Najua kuna watu wengine wanadhani ni utani, huwezi kwenda hata Marekani ukakuta kuna mnyama au mdudu  mwenye bendera ya Marekani,"amesema Diamond.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jocate Mwegelo amesema Diamond ni msanii mkubwa wa kimataifa , hivyo ana nafasi kubwa ya kuielezea dunia kuhusu utalii na fursa ambazo zipo ndani ya Wilaya hiyo.Jokate amefafanua wameamua kuitangaza Kisarawe na kupitia tamasha tamasha Kisarawe kutakuwa na fursa nyingi za utalii na uwekezaji huku akitoa rai kwa mama lishe, baba lishe na wafanyabiashara wengine kujitokeza kwa wingi kufanya biashara wakati wa tamasha hilo kwani kutakuwa na watu wengi.

"Tunataka wote waje viwanja vya Chanzige kwa ajili ya kufanya biashara wakati wa tamasha la Ushoroba likiendelea na hakutakuwa na kiingilio,"amesema Jokate na kusisitiza wakati wa tamasha hilo kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Kisarawe pamoja na wasanii wakubwa akiwemo Diamond.


"Tunataka watu wathamini asili yao, watu wajue asili ya Wazaramu, tunataka watu waje wajionee, waburudike kwani tutakuwa a wasanii wengi wengi katika siku hizo,"amesema Jokate.


01:Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jocate Mwegelo(kushoto) akiwa na Msanii maarufu katika muziki wa Bongo Fleva Nasseb Abdull 'Diamond' baada ya kumkabidhi fulana yenye jina lake kuelekea Kisarawe Ushoroba Festival kuanzia Machi 5 hadi Machi 7 mwaka huu.Diamond ni miongoni mwa wasanii wakubwa watakaokuwepo kwenye tamasha hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jocate Mwegelo(wa tatu kushoto) akizungumza na wananchi wa Wilaya ya hiyo kuelekea Kisarawe Ushoroba Festival ambalo litafanyika kuanzia Machi 5 hadi Machi 7 mwaka huu. Wa pili kulia ni msanii Nasseb Abdull maarufu kwa jina la Diamond ambaye ni miongoni mwa wasanii watakaokuwepo katika tamasha hilo.Wengine kwenye picha hiyo ni viongozi wa wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jocate Mwegelo akiwa na msanii Diamond Platnumz wakielekea kwenye uwanja wa Chanzige ambapo tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival litafanyika kuanzia Machi 5 hadi Machi 7 mwaka huu.

Msanii Diamond Platnumz (wa pili kulia) akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kisarawe kuekelea Kisarawe Ushoroba Festival.(wa tatu kushoto) ni Mkuu wa Wilaya hiyo Jocate Mwegelo. Wengine ni baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jocate Mwegelo akiwa na Msanii Nasseb Abdull 'Diamond' baada ya kutembelea moja ya maeneo ya vivutio vya utalii vilivyopo katika wilaya hiyo. Diamond amekwenda kwenye wilaya hiyo leo kuangalia maandalizi ya kuelekea Kisarawe Ushoroba Festival.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jocate Mwegelo akizungumza na msanii Nasseb Abdull 'Diamond' hayuko pichani, baada ya msanii huyo kufika katika ofisi za mkuu huyo wa wilaya ikiwa ni maandalizi kuelekea Kisarawe Ushoroba Festival.
Msanii Diamond Platnumz akiwasalimia mashabiki wake baada ya kufika kwenye ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.





Msanii Nasseb Abdull 'Diamond' akinunua matunda baada ya kutembelea soko la Kisarawe kuelekea tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...