NA DENIS MLOWE, IRINGA


KUELEKEA maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani Machi 8 mwaka huu, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM) ,Ritta Kabati, amewataka wazazi hususani wanawake kuachana na tamaduni za kisasa katika mfumo wa malezi ya watoto na kurudi katika malezi kwa kuzingatia tamaduni zetu za Kitanzania.

Alisema ifike wakati wazazi wa sasa wakubali kuwa kuna mahali wameteleza warudi katika mila na desturi za Kitanzania zile ambazo ni nzuri za kulea watoto wetu, kuna faida kubwa sana kuliko kuwalea watoto katika tamaduni za wenzetu.

Dkt. Kabati ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa wiki ya Wanawake katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa, iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya sekondari Lugalo na kuratibiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Dkt. Kabati amesema ipo haja ya wazazi kukumbuka namna walivyolelewa katika tamaduni na mila za Kitanzania ambazo kwa asilimia kubwa ziliweza kuwaongoza watoto katika njia bora  iliyowafanya watoto kuwa na heshima na staha katika jamii.

"Ukitafuta sababu kubwa ya mmomonyoko wa maadili kwa vijana wengi sasa, utaona Malezi ya kisasa, kuiga mambo ya wenzetu ambayo sisi si tamaduni zetu. Hapo ndipo tatizo lilipoanzia, Mzazi wa sasa anataka mtoto awe kama mzungu, turudi kwenye njia zetu za Kitanzania ni bora zaidi"

Aidha, Dkt. Kabati ameiasa jamii hususani wazazi Wanawake kuwashirikisha sana watoto na mambo ya Dini kwami kutawafanya watoto waweze kuyajua mazuri na mabaya ambayo Mungu hayapendi na hivyo kupunguza mambo mengi maovu yanayotokea sasa.

"tuwapeleke watoto wetu katika ibada na mafundisho ya dini, hii ni muhimu sana maana watoto kule watajua lipi Mungu hapendi na lipi wafanye kumfurahisha Mungu. Hata sisi wakati tunakuwa tumehimizwa sana mafundisho ya dini, sasa hivi mtoto anajilea mwenyewe hii sio sawa".

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja Wanawake wa CCM (UWT) mkoa wa Iringa, Mama Nicolina Lulandala amewataka Wanawake kuungana katika nyanja ya kiuchumi kwani kufanya hivyo kutawasaidia kuchangia pato la familia na Taifa.

Bi. Lulandala amesema Tanzania ya sasa inamuhitaji mwanamke mjasiriamali ambaye atasaidia Tanzania kufikia malengo ya kuwa na uchumi utegemeao viwanda pamoja na biashara ili kujikwamua kiuchumi katika jamii.

"Tanzania ya sasa inamuhitaji Mwanamke mjasiriamali, Mwanamke atakayeiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa Kati unaotegemea Viwanda. Wanawake tuna nguvu kubwa sana katika kunyanyua uchumi wa familia zetu na Nchi yetu kama tutajitambua katika hilo".

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...