MAMLAKA  ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema kuwa kutokana na umahiri wa maabara zilizopo kwenye Mamlaka hiyo zimeweza kutoa huduma ya upimaji wa sampuli mbalimbali kutoka Katika nchi tofauti za Afrika.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA ,Adam Fimbo katika mkutano maalum na waandishi wa habari kuhitimisha ziara ya siku tatu ya mafunzo kwenye maabara za kisasa zilizopo Dar es salaam kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo .

Amesema kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa na utaratibu wa kukagua na kuthibisha umahili wa maabara mbalimbali Duniani ambapo kwa nchi za Afrika Tanzania ni moja kati ya nchi chache iliyothibitishwa kuwa na maabara zenye ubora hivyo kupelekea baadhi ya nchi za Afrika kuleta Sampuli zao kwaajili ya kuchunguzwa.

"Kuna viwango vilivowekwa na WHO ukifika hicho kiwango wanakutangaza na kukupa cheti hivyo kupelekea nchi nyingine kutaka kujifunza na kuleta Sampuli zao" amesema Fimbo.

Ameongeza kuwa  Nchi hizo ni pamoja na Zambia, Lesotho, Malawi, Uganga na Kenya na kwamba hilo limewezekana kutokana na tangazwa na WHO. 

Ziara hiyo ya siku tatu imehitimishwa rasmi Machi 5,2021 kwa waandishi wa habari kutembelea maabara ya Dawa na Vifaa Tiba nyongeza kwa kuangalia maabara maalumu ya MICROBIOLOGY inayotumika kupima vifaa tiba mbalimbali ikiwemo Barakoa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano maalum wa kuhitimisha ziara ya siku tatu ya mafunzo kwenye maabara za kisasa zilizopo kwenye Ofisi zao  leo Dar es Salaam. kushoto Meneja wa Elimu ya Umma na Mawasiliano wa TMDA, Gaudensia Semwanza.
Meneja wa Elimu ya Umma na Mawasiliano wa TMDA, Gaudensia Semwanza (kushoto) akizungumza na waandishi wakati wa kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu kuzungumza na waandishi hao leo Dar es Salaam.
Mchunguzi wa Maabara  TMDA,Gerald Sambu  akufafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa ziara ya kutembea Maabara hiyo leo Dar es Salaam.
Mchunguzi wa Maabara wa TMDA Olson Mkeya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika Maabara Maalum ya MICROBIOLOGY inayotumika kupima vifaa tiba mbalimbali ikiwemo Barakoa leo Dar es Salaam.Waandishi wa habari wakimsiliza Mchunguzi wa Maabara  TMDA,Gerald Sambu wa (kulia)  leo Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
kazi ikiendelea 
Muonekano wa Maabara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...