Kampuni inayotengeneza mabomba ya maji ya Plasco Limted ya Dar es Salaam nchini imetakiwa kusambaza teknolojia yake mpya ya Weholite, inayookoa muda na fedha nyingi za serikali huku pia wakitakiwa kuongeza uzalishaji wa mabomba.

Pia wametakiwa kusambaza mabomba hayo yenye viwango vya ubora unaotakiwa kwa haraka, kwa sababu kuna miradi zaidi ya 600 ya maji inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbali mbali nchi nzima.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwenye ofisi za kampuni hiyo, jijini Dar es Salaam alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea Makampuni na Viwanda vinavyotengeneza vifaa vya kusambaza majisafi na majitaka nchini akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo amesema wakandarasi wengi nchini wa miradi ya maji, wamekuwa wakilia na ukosefu wa mabomba kwamba hayapatikani, wakati kuna makampuni kadhaa nchini ikiwemo Plasco, yanatengeneza mabomba mengi na yenye viwango bora.

"Anzisheni miradi ya maonyesho katika maeneo mbalimbali Onyesheni hiyo teknolojia yenu mpya ya kutengeneza mabomba ya Weholite hasa katika maadhimisho ya Wiki ya Maji baadaye mwezi huu...,  ikionekana wataalamu wetu wataiona na watasaidia kuisambaza katika maeneo mengi nchini” amesema Aweso.

Aidha waziri Aweso ameeleza kufurahishwa kwake na maendeleo makubwa yanayofanywa na kampuni hiyo ya Plasco na kuongeza kuwa,  kuanzia sasa hataraji kusikia makandarasi wakisingizia ukosefu wa mabomba, kwamba ndiyo yanawakwamisha kukamilisha miradi, kwa sababu katika ziara yake leo jijini Dar es Salaam, amebaini kuwa mabomba yanapatikana kwa wingi.

Amesema kama kuna mkandarasi ataendelea kusingizia ukosefu wa mabomba, basi aondolewe katika miradi, badala yake wizara itatumia wataalamu wake ambapo kwa kutumia wataalamu wake, wizara imeokoa fedha nyingi na kuiwezesha  kwa muda mfupi kutekeleza miradi 192 iliyokwama.

Ameongeza kuwa, miradi hiyo kama ingeendelea kutekelezwa na makandarasi waliojaa visingizio visivyokwisha, ingegarimu Sh. bilioni 207 lakini kwa kutumia wataalamu wake  Wizara imetumia Sh bilioni 193 na kuwawezesha kuokoa mabilioni ya fedha za serikali.

Wateja wakubwa wa Kampuni ya Plasco ni Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) na mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira za miji mbalimbali nchini. Asilimia 80 ya wateja wa Plasco ni serikali na taasisi zake.

KWa upande wake  Afisa Uendeshaji wa Kiwanda cha Plasco, Alimiya Osman amesema wanafurahi kutembelewa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Uongozi mzima wa RUWASA na DAWASA na kuahidi kuendelea kushiriana kwa ukaribu zaidi na wizara hiyo ili kuongeza ufanisi katika kazi zao.

Amesema kwa sasa  wanazalisha malighafi za tani 28,000 kwa mwaka ambapo katika tani hizo asilimia 70 ni mabomba ya plastiki.

Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kiwanda cha Plasco Ltd, Alimiya Osman (kulia) akimwonyesha Waziri wa Maji, Jumaa Aweso mabomba ya kisasa na yenye ubora aina ya Weholite yanayotumika katika miradi mikubwa ya maji na ujenzi wa miundombinu ya barabara  alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Chang'ombe Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Plasco Ltd inayozalisha mabomba ya Maji wakati alipotembelea kiwanda hicho, jijini Dar es Salaam leo
Waziri wa Maji Juma Aweso,akijaribu kutumia moja ya mashine inayotumika katika utengenezaji wa bomba aina ya Weholite.
Waziri wa Maji Juma Aweso, akimzawadia kiasi cha fedha Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Plasco Ltd inayotengeneza mabomba ya Maji. Edith James baada ya kuridhishwa na maelezo ya kitaalamua kuhusu uzalishaji na mauzo ya mabomba ya kampuni hiyo.
Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kiwanda cha Plasco Ltd, Alimiya Osman,akielezea jambo kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alipotembelea kiwanda hicho kinachozalisha mabomba ya kisasa na yenye ubora aina ya Weholite yanayotumika katika miradi mikubwa ya maji na ujenzi wa miundombinu ya barabara wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Chang'ombe Dar es Salaam leo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...