RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi asalimiana na Viongozi wa Serikali alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, kuhudhuria ufunguzi wa Kongamano la Kujadili Matumizi ya Sekta ya Mawasiliano ya Habari katika kuijenga Zanzibar Mpya, lililofanyika leo 1-3-2021

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akielekea katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, kuhudhuria hafla ya Ufunguzi wa Kongamano la Waandishi wa Habari Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Kamati ya Waandishi wa Habari Zanzibar Ndg. Farouk Karim.

MWENYEKITI wa Kamati ya Waandishi wa Habari Zanzibar Ndg, Farouk Karim akizungumza na kutowa maelezo ya lengo la Kongamano la Waandishi wa Habari Zanzibar la Kujadili Matumizi ya Sekta ya Mawasiliano ya Habari Katika Kuijenga Zanzibar Mpya, kabla ya ufunguzi wa Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akipiga makofi wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Waandishi wa Habari Ndg.Farouk Karim, akitowa maelezo ya Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita.

MUWASILISHAJI Mada ya Mapendekezo ya Wadau wa Habari Dhidi ya Mswaada wa Habari Zanzibar ikiwasilishwa na Bw. Suleiman Seif, wakati wa Kongamano la Waandishi wa Habari Zanzibar Kujadili Matumizi ya Sekta ya Mawasiliano ya Habari katika Kuijenga Zanzibar Mpya, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

WAZIRI wa Habari,Vijana Utamadini na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Waandishi wa Habari Zanzibar kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, kulifungua Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamano la Waandishi wa Habari Zanzibar Kujadili Matumizi ya Sekta ya Mawasiliano ya Habari katika Kuijenga Zanzibar Mpya, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

 

 

WAANDISHI wa Habari Waandamizi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Kongamano la Waandishi wa Habari Zanzibar Kujadili Matumizi ya Sekta ya Mawasiliano ya Habari katika Kuijenga Zanzibar Mpya, lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Waandishi wa Habari Zanzibar walioandaa Kongamano hilo waliosimama nyuma, na waliokaa kutoka (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita ,Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar.Dkt.Abdalla Juma Mabodi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na Waandishi wa Habari Waandamizi Zanzibar waliosimama nyuma, na waliokaa kutoka (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita ,Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar.Dkt.Abdalla Juma Mabodi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana.

(Picha na Ikulu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...