Na Amiri Kilagalila,Njombe

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) anatarajia kuwasili mkoani Njombe jumatano tarehe 10 Machi,2021 kwa ziara ya kikazi ya siku nne.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake,mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Lubirya amesema katika ziara hiyo waziri mkuu atashiriki mkutano wa wadau wa zao la chai uliondaliwa na wizara ya kilimo kwa kushirikiana na bodi ya chai  huku siku ya Alhamisi ataitumia siku hiyo katika ukaguzi wa bara bara Njombe kuelekea wilayani Ludewa – Manda na bandari ya Manda.

Aidha amesema akiwa njiani atapokea taarifa ya ujenzi wa bara bara sehemu ya Lusitu –Mawengi yenye urefu wa Kilomita 50 inayojengwa kwa kiwango cha zege ya saruji. 

“Mtakumbuka miezi miwili iliyopita kuna meri ambayo imezinduliwa kule Ruvuma ambayo inafanya safari zake ndani ya Ruvuma na Kyera kule mkoani Mbeya lakiini inapita katika bandari iliyoko mkoani mwetu,kwa hiyo bandari ya Manda ni sehemu ambayo itatembelewa na Mh,Waziri mkuu wakati akiwa mkoani mwetu”alisema Lubirya

Vile vile amesema siku ya Ijumaa waziri mkuu ataweza kurejea wilaya ya Njombe na kupata fursa ya kutembelea mashamba ya parachichi kutokana na mkoa wa Njombe kwa sasa kukua katika kilimo hicho.

Lubirya ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kumpokea kiongozi huyo wa kitaifa atakapokuwa njiani kuja Njombe na maeneo yote atakayopita wakati wa ziara yake.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...