Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amekutana na Viongozi wa Vyombo vya habari vya taasisi za Dini nchini (TAREMA - Tanzania Religious Media Association) Kujadili juu ya changamoto ya Leseni za usajili wa vyombo vya vya habari vya taasisi za kidini Nchini. katika  Ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) 15 April 2021.


Pamoja na mambo mengine Mhe. Bashungwa amesikikiza maoni na changamoto mbalimbali ili kupatiwa majibu na ufafanuzi wa kisera utakaosaidia kuendesha taasisi  hizo mihimu zinazojenga jamii kimaadili kupitia mafundisho ya kiroho na kiimani.

 

Mwenyekiti wa TAREMA, Dr. Vernon Fernandes ameanza kwa kutoa pole kwa Serikali na Wananchi kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli huku akipongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimalisha amani ya nchi.

 

Baadhi ya Maombi na Changamoto yaliyowasilishwa na  Makamu Mwenyekiti wa TAREMA, Sheikh Hassan A. Hassan kwa niaba ya viongozi wote ni Kuomba TCRA irudishe Lesini za vyombo vya habari visivyo vya kibiashara (Non - Commercial broadcasting Licenses) na TCRA iweke utaratibu wa kukutana  na wamiliki wa vyombo vya habari kwa lengo la kufahamishana mabadiliko ya sera na sheria kabla ya wadau kuanza kuzitumia.

 

Aidha, Mhe. Bashungwa baada ya kusikiliza maoni na changamoto hizo, ameanza kwa kuvipongeza viongozi wa vyombo vya habari vya taasisi za dini nchini kwa kazi kubwa waliyojitoa kuifanya ambayo imekuwa msaada kwa Taifa kwa kutoa mafundisho ambayo wamekuwa wakitoa kupitia kupia TV, Radio na Magazeti ambayo wamekuwa wakiyasimamia.

 

Wakati akijibu hoja na changamoto mbalimbali, Mhe. Bashungwa ameelekeza uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano - TCRA kukukaa mara moja na viongozi hao ili kufanyia kazi maoni yaliyowasilishwa kwake huku akiwaagiza kila mwaka kuwa na mkutano utakaowakutanisha na wadau wao ili maamuzi yatakayofanyika yatumike katika mabadiliko na sera pamoja na uendeshwaji wa vyombo vyao vya habari.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...