Charles James, Michuzi TV

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amefanya ukaguzi maalum katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kubaini kuwepo kwa mapungufu kadhaa ikiwemo upotevu wa mapato kwa kutoa msamaha usiostahili wa Dola za Marekani 979,126.5 kwa Kampuni ya Saruji ya Mbeya.

Hayo yamebainishwa katika taarifa ya CAG aliyoisoma leo kwa wandishi wa habari jijini Dodoma ambapo ambaini pia kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha na ubadhirifu wa malipo ya Sh Bilioni 3.76.

Akizungumzia ukaguzi huo wa TPA, CAG Charles Kichere amesema April 30, 2018 menejimenti ya TPA ilipeleka kwenye Bodi ya Usimamizi maombi ya msamaha wa Dola za Marekani Milioni 1.52 kuiombe kampuni ya saruji Mbeya kwa ajili ya wateja wake waliopo Burundi na DR Congo wanaosafirisha saruji kupitia Bandari ya Kasanga.

Amesema Kampuni hiyo ilieleza kuwa wateja wao walipata changamoto ya kukosa meli za kuja Bandari ya Kasanga kuchukua shehena za saruji zao walizokua wameagiza na hivyo kupelekea shehena hiyo kuharibika.

Amesema April 17, 2019 kupitia azimio la Bodi ilitoa msamaha wa asilimia 100 kama ilivyoombwa hivyo kampuni hiyo ya Saruji Mbeya ilipaswa kulipa Dola za Marekani 50,000 kama gharama za utunzaji wa shehena hizo na Dola za Marekani 7,726 kwa ada tu ya kuondolea shehena.

CAG Kichere amesema ukaguzi wake uliangalia ukweli wa msamaha uliotolewa na uligundua shehena ya tani 1,445 (mifuko 28,904) ambayo iliharibika katika Bandari ya Kasanga ilikua na malimbikizo ya gharama ya Dola za Marekani 543,224 iliyostahili kutolewa msamaha.

" Maombi ya msamaha yaliyopelekwa katika Bodi April 14, 2019 yalikua ya Dola za Marekani Milioni 1.52 yakijumuisha madeni ya saruji iliyoharibika ya Dola za  Marekani 543,244 na gharama za utunzaji Dola za Marekani 979,126 kwa shehena zilizosafirishwa kutoka Bandari ya Kasanga katika kipindi cha Januari 2013 na Oktoba 2017 na hakukua na hasara iliyopatikana na hivyo  kutostahili msamaha.

Kuchukulia shehena nzima ya tani 1445.2 kama imeharibika na kutoa msamaha wa Dola za Marekani Milioni 1.52 badala ya gharama sahihi ya Dola 543,244 kuliisababishia hasara TPA ya upotevu wa mapato wa Dola za Marekani 979, 126.59.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...