JESHI la Polisi la kanda maalum ya Dar es salaam linaendelea kuchunguza tuhuma za kusambaa picha za utupu za msanii wa Muziki wa kizazi kipya Rajab Abdul Kahal maarufu kama Harmonize, ambaye picha zake za utupu zimesambaa katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkoani Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa amesema  jeshi la polisi linaendelea kuchunguza sakata la kusambaa kwa picha za utupu la msanii tajwa ambaye ametoa malalamiko baada ya kusikia picha hizo zimesambazwa na watu ambao hawamtakii mema katika shughuli yake.

Amesema washukiwa wa sakata  la kusambaza picha hizo wamekamatwa na kuhojiwa na baada ya kutimiza vigezo vya dhamana waliachiwa jana jioni na upelelezi unaendelea na ukikamilika jalada litapelekwa kwa wakili wa serikali wa kanda na akibainisha jinai watuhumiwa watapelekwa mahakamani.

 Aidha SACP Mambosasa amesema, wasanii wamekua watumiaji wabaya wa mitandao ya kijamii kwa kuhasimiana kundi na kundi kwa kujaribu kushushana katika biashara ya Muziki.

"Niwaonye wasanii, tunawaheshimu mnafanya kazi nzuri ya sanaa ila waheshimu ajira zao na kujiuliza wanayoyafanya kabla ya kutenda, hatutamwangalia mtu kwa heshima yake akitenda kosa atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria kama wahalifu wengine.'' Amesema Mambosasa.

Pia  amewaonya watumiaji wa simu na mitandao ya kijamii kulinda na kuheshimu mila na tamaduni za kitanzania, hasa kwa kumpiga mtu picha ya utupu na kuirusha katika mitandao ya kijamii.

Kufuatia sakata hilo la kusambaa kwa picha za utupu za msanii wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize hadi sasa  watuhumiwa watano wamehojiwa akiwemo msanii wa Filamu Frida Kajala Masanja(36,) Paula Paul Pter (18,) Raymond Shabani Mwakyusa maarufu kama Rayvanny  (27,) Claiton Revocatus (34,) maarufu kama Baba Levo, Catherine John Charles na Juma Haji (32) na baada ya kuhojiwa watuhumiwa wote wapo nje kwa dhamana. 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...